Ukaribisho wa Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kwa niaba ya Watumishi na Wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ninayofuraha kubwa kukukaribisha katika tovuti hii ambako tunaimani kubwa utapata taarifa za kuaminika na shughuli zinazofanyika katika Halmashauri ya Wilaya Karagwe.Kama taasisi ya Serikali tunaamini katika uwazi,ukweli na uwajibikaji kwenye utendaji wetu wa kila siku.
Aidha kwa kutambua umuhimu wa wateja tunaowahudumia zipo taarifa na fomu mbalimbali ambazo zinakuwezesha kupata huduma moja kwa moja kwenye tovuti.
Hii inahusisha upatikanaji wa leseni za biashara na leseni za vileo na taarifa mbalimbali.Ni matumaini yangu utatumia tovuti hii kupata taarifa muhimu na kwa malalamiko,mapendekezo basi usisite kuwasiliana nasi na kutumia tovuti yetu kutoa malalamiko yako nasi tutakufikia.
Karibu Halmashauri ya Wilaya Karagwe, Halmashauri yenye fursa za maendeleo kwako na kwa Taifa
KARIBU SANA.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.