DKT.DUGANGE ABARIKI MRADI WA KUDHIBITI TAKA NGUMU KARAGWE DC, AZINDUA GARI MAALUM KWAAJILI YA KUKUSANYA, KUSAFIRISHA, KUTUNZA NA UTUPAJI SALAMA.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Festo John Dugange ameubariki rasmi mradi wa kudhibiti taka ngumu unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwa kushirikiana na Manispaa ya fourth nchini Ujerumani kwa kuzindua gari maalum litakalokuwa likikusanya na kusafirisha taka hizo kwa ajili ya utunzaji na utupaji salama.

Akizungumza hapo jana Februari 26, 2026 katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Dkt. Dugange ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa utunzaji wa Mazingira, huku akitoa wito kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuendelea na hatua zinazofuatwa ikiwemo kujenga vizimba kwa ajili ya ukusanyaji taka na kuhakikisha utenganishwaji wa taka unazingatiwa na gari kuanza kufanya kazi.

“Nimekuja kuwashirikisha kuhusiana na fursa za taka, Taka ni Mali leo tunajua Wananchi wananufaika na taka za makopo ya maji ya plastick lakini tunazo taka maarufu ‘Taka oza’ zile zinazopatikana masokoni. Serikali imekuja na mpango mzuri kuhakikisha inajenga mitambo ya kuchakata taka hizi na kuzalisha mbolea asili nzuri. Pia, kunafursa ya biashara ya hewa ya ukaa ‘Kaboni’ Wataalamu wetu wataendelea kutoa Elimu na sisi Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) tumedhamiria kuhakikisha tunanufaika na hili” Alisema Dkt. Dugange.

Aidha, Dkt. Ndugage alipata nafasi ya kutembelea mradi wa vijana (Kiuma) wa uchakataji taka ngumu na uhifadhi wa mazingira, mradi wa maji taka unaotekelezwa na Buwasa pamoja na Mradi wa hewa ya ukaa na shamba la mkahawa linalomilikiwa na Kaderesi lililopo kata ndama Wilayani humo lengo ni kuhimiza utunzaji Mazingira pamoja na uwekezaji wa hewa ukaa.

Hatahivyo, Dkt. Dugange alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza Wananchi wa Tanzania kuendelea kuuenzi na kuusemea muungano na kuhamasisha mashuleni watoto wajifunze umuhimu wa muungano wa (Tanganyika na Zanzibar). Pia, amewaomba viongozi wote kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa agenda ya umuhimu wa Muungano iwe ya kudumu.

KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.