Utengamano/Uadilifu: Kuzingatia Kanuni na Maadili ya utendaji mzuri wa majukumu na uwajibikaji yaliyotolewa kwa mtumishi husika.
Heshima: Daima ripoti kwa Taasisi ambayo inapaswa au imepangwa kutembelewa na huduma za Taasisi hiyo zinahitaji msaada wa usimamizi ili kuhakikisha mahusiano mazuri.
Wajibu na Uwajibikaji: Hakikisha kuwa kazi uliyopangiwa inafanyika kwa kiwango kinachohitajika na kutolewa taarifa kwa usahihi;
Matokeo Tarajiwa: Utendaji unaozingatia matokeo chanya na yanayotarajiwa na mteja au mpokea huduma.
Utayari : Kuwa na utayari wa kukabiliana na hali yoyote inayonufaisha Jamii yenye uhitaji wa Mabadiliko.
Uelewa wa jinsia: Kuzingatia usawa wa kijinsia kwa Wanawake na Wanaume.
Ari ya kufanyakazi kwa umoja: Kuwa na utamaduni wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa unaolenga ufanisi wa utendaji na kufikia lengo la Taasisi.