MAJUKUMU YA KITENGO CHA UCHAGUZI
Katika kipindi hiki cha mwaka 2016/2017 kitengo cha Uchaguzi kimeendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida. Shughuli zilizofanyika katika kipindi hiki ni kama ifuatavyo.
Kufuatilia kesi za uchaguzi zilizopo mahakamani za uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 na uchaguzi Mkuu 2015
Kuhudhuria vikao mbalimbali vya kikazi
Kuratibu nafasi wazi za viongozi wa kata , Vijiji na Vitongoji
Kusimamia’ Hesabu za mali (Stock taking) ya vifaa vya uchaguzi
2.0 UTEKELEZAJI
2.1 Kufuatilia kesi za uchaguzi zilizopo mahakamani za uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 na uchaguzi Mkuu 2015.
Jumla ya kesi 3 za uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 bado zipo mahakama kuu katika hatua ya usikilizwaji; na kesi 1 ya uchaguzi mkuu ,2015 wa madiwani nayo iko mahakama kuu kwa hatua ya usikilizaji.
Kuratibu nafasi wazi za viongozi wa kata , vijiji na vitongoji
Kwa mwaka 2016/17 jumla ya nafasi 54 za viongozi wa vijiji ziko wazi kutokana na sababu mbalimbali kama inavyoonekana katika jedwali hapo chini .Aidha kulingana na maelekezo tuliyoyapata toka Ofisi ya katibu tawala Mkoa kwa barua kumb Na.FA.78/148/01’D’/56 ya Tarehe 06/12/2016 uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi za viongozi wa vijiji na kata unagharimiwa na Halmashauri husika. Katika bajeti ya 2016/17 ziliidhinishwa Tsh. 10,017,000 makisio halisi ni Tsh. 20,385,000.00. Hivyo ufanyikaji wa uchaguzi mdogo utategemea upatikanaji wa fedha.
kusimamia Hesabu za mali (Stock taking) ya vifaa vya uchaguzi
kazi hii imefanyika tarehe 10 Juni,2017 kwa kushirikiana na kitengo cha manunuzi na ugavi.
Jedwali A: Nafasi wazi za Viongozi wa Vijiji na Vitongoji kwa mwaka 2016/2017
NA
|
NAFASI WAZI
|
Kata
|
KIJIJI/KITONGOJI
|
SABABU
|
1
|
Mwenyekiti wa Kijiji
|
Kanoni
|
Rwambaizi
|
ametenguliwa katika nafasi hiyo baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja
|
2
|
Wajumbe 4 Halmashauri a Kijiji
|
Kanoni
|
Rwambaizi
|
1-kuondolewa dhamana na chama
-3 kujiuzuru |
3
|
Mwenyekiti wa kitongoji
|
Kanoni
|
Rwambaizi/Omurwele
|
Alijiuzuru
|
4
|
Wajumbe 4 Halmashauri ya Kjiji
|
Kanoni
|
Kibona
|
Kujiuzuru na kuhama
|
5
|
Wajume 5 Halmashauri ya kijiji
|
Kanoni
|
Kanoni
|
Kujiuzuru na kuhama
|
6
|
Wajumbe 4 Halmashauri ya Kjiji
|
Kanoni
|
Nyakahita
|
1-amefariki
1-amejiuzuru 2- wamehama |
7
|
Mwenyekiti wa Kijiji
|
Rugu
|
Kasheshe (Rugu)
|
Amefariki
|
8
|
Mjumbe wa Serikali ya Kijiji
|
Kasheshe (Rugu)
|
Ameenda masomoni na kujiuzuru
|
|
9
|
wenyekiti wa vitongoji
|
Kihanga
|
Kihanga/bugerelo
|
wamefariki
|
10
|
Mjumbe serikali ya kijiji
|
Kihanga
|
Kibwera
|
Amefariki
|
11
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Kihanga
|
Kishoju/miembeni
|
Amefariki
|
12
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Bweranyange
|
Bweranyange/omukatukuru
|
Amefariki
|
13
|
Mwenyekiti wa Kijiji
|
Bweranyange
|
Chamchuzi
|
Amefariki
|
14
|
Mwenyekiti wa kitongoji
|
Kituntu
|
katembe/Kitongoji Rushe 'A'
|
Amejiuzuru
|
15
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Kituntu
|
katwe/Nyakigongo 'B'
|
Kupata hatia na kufungwa miaka miwili
|
16
|
Wajume 2 wa serikali ya kijiji
|
Kituntu
|
Katembe
|
Kutohudhuria vikao vya kisheria tangu achaguliwe
|
17
|
Mwenyekiti wa kitongoji
|
Kituntu
|
Katembe/bikiri
|
Aliondolewa dhamana na chama
|
18
|
Mjumbe 1 serikali ya kijiji
|
Kituntu
|
katwe
|
alijiuzuru
|
19
|
Mjumbe 1 serikali ya kijiji
|
Kituntu
|
Kituntu
|
alijiuzuru
|
20
|
Mwenyekiti wa Kijiji
|
Nyakakika
|
Kanywamagana
|
Alijiuzuru
|
21
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Nyakakika
|
KAIHO/Ahakatoma
|
Kushindwa kesi mahakamani
|
22
|
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji
|
Rugera
|
Nyarugando
|
Amejiuzuru
|
23
|
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji
|
Omukakajinja
|
Amejiuzuru
|
|
24
|
Mwenyekiti wa Kijiji
|
Kiruruma
|
Biyungu
|
Amefariki
|
25
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Kiruruma
|
Kiruruma/ Kalamba
|
Amefariki
|
26
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Kayanga
|
Rwambale
|
Amepoteza sifa
|
Hakuonekana kwenye Kitongoji chake kwa miezi saba mfurulizo
|
||||
|
||||
27
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Nyakabanga
|
kanogo/chanyamuromba
|
Amefungwa mwaka mmoja gerezani
|
28
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Nyakabanga
|
kanogo/rwakihigwa
|
Amefungwa mwaka mmoja gerezani
|
29
|
Mwenyekiti wa kijiji
|
Ihembe
|
Kibogoizi
|
amefariki
|
30
|
Mjumbe wa halmashauri ya kijiji
|
Ihembe
|
Kibogoizi
|
Amefariki
|
31
|
Mwenyekiti wa kitongoji
|
Ihembe
|
Ihembe II/Kibembe
|
Amefutiwa dhamana na chama chake
|
32
|
Mwenyekiti wa kitongoji
|
Chanika
|
Kahundwe/champesha
|
Haonekani kwenye kituo cha kazi
|
33
|
Mjumbe wa Halmashauri ya kijiji
|
Chanika
|
Kahundwe
|
Kutohudhuria vikao vya kisheria tangu achaguliwe
|
34
|
Wajumbe 3 halmashauri ya kijiji( viti maalum)
|
Nyabiyonza
|
Bukangara
|
kuhama na kujiuzuru
|
35
|
Wajumbe 3 halmashauri ya kijiji
|
Nyabiyonza
|
Nyabiyonza
|
kujiuzuru
|
36
|
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Nyabiyonza
|
Ahakishaka /ahakishaka
|
amefariki
|
30 |
Mwenyekiti wa Kitongoji
|
Nyakasimbi
|
Kahanga/kahanga
|
Kuacha na kwenda masomoni
|
3.0 Changamoto
katika kipindi hiki kitengo kimekabiliwa na changamoto ya kushindwa kuteketeza nyaraka za chaguzi zote mbili kutokana na kuwepo kwa kesi mahakamani na pia kutopata mwongozo wa uteketezaji wa nyaraka za uchaguzi wa serikali za mitaa.
Afua ya kukabiliana na changamoto hizo: kufuatilia kwa karibu kesi zilizopo mahakamani ili zikamilike . Hata hivyo kitengo kinaendelea kuwasiliana na mamlaka za juu ili kuona namna ya kutelekeza nyaraka kwa maeneo ambayo hayana kesi na pia kupata mwongozo wa uteketezaji wa nyaraka za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2014.
Ashura A. Kajuna
MKUU WA KITENGO CHA UCHAGUZI
HALMASHAURI YA WILAYA
KARAGWE
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.