SECONDARY EDUCATION
The district has a total of 36 Secondary Schools with a total of 18583 students (7138 Boys and 9445 Girls).
The issue of rehabilitation and construction of classrooms and teacher houses have been an importantfocus. The strategy for construction of classrooms and teachers’ houses has changed from a true paidconstruction to cost sharing arrangement with community contribution taken to the maximum. This hasproved to be an effective and cost efficient strategy to increase the number of classrooms, teachers’ houses, and latrines. It has also reinforced community ownership of schools and capabilities inaddressing problems.
CLASSROOM TEACHERS RECRUITMENT AND DEPLOYMENT
For the year 2024, the Secondary Education division has a total of 506 teachers in 28 Government schools. There is a shortage of 190 teachers (144 science teachers and 46 social studies teachers)
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA IDARA YA ELIMU YA SEKONDARI KWA MWAKA 2023/2024
1.0 UTANGULIZI
Wilaya ina jumla ya Shule za Sekondari 36 zenye jumla ya wanafunzi 18583 (Wavulana 7138 na Wasichana 9445 kama ilivyochanganuliwa kwenye jedwali lifuatalo.
IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI NA WANAFUNZI
KWA MWAKA 2024
SHULE |
IDADI YA SHULE |
WAVULANA |
WASICHANA |
JUMLA |
SHULE ZA SERIKALI
|
28
|
7,201
|
8,123
|
15,324
|
SHULE ZA BINAFSI
|
08
|
1,937
|
1,322
|
2,259
|
JUMLA KUU
|
36
|
9,138
|
9,445
|
18,583
|
1.1 IDADI YA WALIMU
Kwa mwaka 2024 divisheni ya Elimu sekondari ina jumla ya walimu 506 katika shule 28 za Serikali. Kuna upungufu wa walimu 190 (Walimu wa masomo ya Sayansi ni 144 na wa masomo ya jamii ni 46).
1.2 IDADI YA WATUMISHI MAKAO MAKUU
Wapo jumla ya 4
2.0 MIUNDOMBINU MUHIMU
Ifuatayo ni hali halisi ya uwepo wa miundombinu katika shule za Sekondariza Serikali.
Na.
|
AINA YA MAJENGO |
MAHITAJI |
UPUNGUFU |
% |
1
|
Madarasa
|
408 |
34 |
8.3 |
2
|
Matundu ya vyoo wanafunzi
|
670 |
338 |
50 |
3
|
Matundu ya Vyoo walimu
|
63 |
25 |
39 |
4
|
Nyumba za walimu
|
506 |
400 |
79 |
5
|
Majengo ya Utawala
|
28 |
10 |
35 |
6
|
Maktaba
|
28 |
15 |
53 |
7
|
Bwalo
|
28 |
25 |
89 |
8
|
Hostel – Wav
|
28 |
20 |
71 |
9
|
Hostel-Was
|
28 |
20 |
71 |
10
|
Vyumba vya maabara
|
78 |
44 |
56 |
11
|
Majiko
|
28 |
20 |
71 |
2.1 MIUNDOMBINU INAYOENDELEA KUJENGWA HADI SASA
2.1.1 Ujenzi wa shule mpya ya Mkoa ya Wasichana Kagera River kwa jumla ya Tshs. 4,100,000,000/= toka SEQUIP.
2.1.2 Ujenzi wa shule mpya ya Kata ya Bugene kwa jina Omurushaka Sekondari kwa jumla ya Tshs. 584,029,000/= toka SEQUIP.
2.1.3 Ujenzi na ukamilishaji wa madarasa na matundu ya vyoo kwa Tshs. 125,000,000/= toka SEQUIP kwa shule za Kituntu, Nono, Kayanga, Nyakahanga, Kiruruma na Chakaruru.
2.1.4 Pia idara imepokea jumla ya Tshs. 2,085,000,000/= Januari, 2024 za ujenzi wa vyumba vya madarasa 63, ukamilishaji ujenzi wa vyumba vya madarasa 18 na ujenzi wa matundu ya vyoo 88 katika shule za sekondari 18.
3.0 UWEPO WA VITABU SHULENI
Vitabu shuleni vinanunuliwa kwa fedha ya Elimu (Capitation grand). Hadi Januari 2024 uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi kwa masomo ya Sayansi ni 1:2 na masomo ya sayansi jamii ni 1:3.
4.0 CHANGAMOTO
4.1 Upungufu wa watumishi unaoathiri utendaji kazi. Kuna upungufu wa walimu 190 ikiwa walimu wa masomo ya Sayansi 146 na masomo ya Sayansi jamii ni 46. Aidha hakuna Afisa Elimu Watu Wazima.
4.2 Upungufu wa miundumbinu muhimu kama vile nyumba za walimu, hosteli, majengo ya utawala, maktaba na samani.
4.3 Ukosefu wa watumishi wa kuajiriwa upande wa kada za uhasibu, ukarani, uboharia, ulinzi, upishi na Mwandishi Mwendesha Ofisi (Secretary).
4.4 Jamii kutoona muhimu sana wa kuchangia chakula shuleni kwa watoto wao na hivyo kupelekea wanafunzi kusoma wakiwa na njaa. Hii husababisha utoro na kuporomoka kwa ufaulukatika mitihani mbalimbali ikiwemo ya Taifa.
4.5 Baadi ya shule kukosa viwanja vya michezo kutokana na mazingira, pia ufinyu wa maeneo.
5.0 MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU KATIKA SHULE ZA SEKONDARI
Kwanza ni jambo la kujivunia kuwa ufuulu unapanda kwa mwaka. Mwaka 2023 matokeo ufaulu ni 94.4% na kidato cha nne ni 95%. Lengo la Taifa ni ufaulu wa 85% Divisheni ya Elimu Sekondari inalenga kuboresha Elimu hasa kupandisha ufaulu kwa kutumia mikakati ifuatayo:-
5.1 Kuendelea kuelimisha jamii kuwa jukumu la kujenga au kukamilisha miundombinu shuleni ni la wananchi wote.
5.2 Kutoa elimu kwa jamii/wazazi/walezi kuchangia chakula shuleni cha watoto wao.
5.3 Kufanya ufuatiliaji shuleni wa mara kwa mara ili kuhakikisha walimu wanafundisha ipasavyo na kutatua matatizo yao kwa wakati.
5.4 Kuomba Serikali iajiri walimu pungufu na kuhamasisha jamii kuendelea kuajiri walimu na watumishi wengine wa muda.
5.5 Kufundisha kwa bidii na kukamilisha mada kikamilifu kwa muda.
5.6 Kufanya mitihani ya majaribio nay a ushindani ili kuwapima na kuamsha ari ya wanafunzi katika usomaji na ujifunzaji.
5.7 Kuhimiza na kuhamasisha michezo shuleni.
Mwl. JOHNBOSCO PAUL
KNY; AFISA ELIMU SEKONDARI
HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.