KITENGO CHA TEHAMA:
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni mojawapo ya vitengo tisa (09) na Idara tisa (09) zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Kitengo cha TEHAMA kina jumla ya watumishi watatu (03) ambao ni kama ifuatavyo:-
Na
|
Jina la Mtumishi
|
Cheo
|
01.
|
Adam Kiunsi John
|
Afisa TEHAMA
|
02.
|
Rukiza Abed Rwakilomba
|
Afisa TEHAMA
|
03.
|
Aliko John Mwambegele
|
Afisa TEHAMA
|
Kitengo cha TEHAMA cha TEHAMA kinahusika moja kwa moja na mifumo yote katika Halmashauri.Ifuatayo ni mifumo inayosimamiwa na kitengo cha TEHAMA.
NA
|
JINA LA MFUMO
|
IDARA/KITENGO MFUMO UNAPOTUMIKA
|
1.
|
Mfumo wa malipo Serikalini (MUSE)
|
Kitengo cha Fedha na Kitengo cha Ugavi
|
2.
|
Mfumo wa Taarifa za kiutumishi (HCMIS)
|
Divisheni ya Utawala na Utumishi
|
3.
|
Mfumo wa huduma za matibabu (GoTHoMIS)
|
Divisheni ya Afya.
|
4.
|
Mfumo wa kupokea na kutolea taarifa za kifedha ngazi ya vituo (FFARS)
|
Divisheni ya Elimu Msingi, Sekondari na Afya
|
5.
|
Mfumo wa mapato (TAUSI)
|
Kitengo cha Fedha na Idara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji.
|
6.
|
Mfumo wa mapato (LGRCIS)
|
Kitengo cha Fedha na Idara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji.
|
7.
|
Mfumo wa Bajeti (Planrep)
|
Divisheni ya mipango, takwimu na ufatiliaji.
|
8.
|
Mfumo wa sensa za elimu msingi na sekondari (BEMIS)
|
Divisheni ya Elimu msingi na sekondari.
|
9.
|
Mfumo wa manunuzi (NEST)
|
Kitengo cha Ugavi na manunuzi
|
10.
|
Mfumo wa huduma za kiutumishi (ESS)
|
Divisheni na vitengo vyote vya Halmashauri.
|
4.0 MAJUKUMU YA KITENGO CHA TEHAMA
Kutayarisha mpango mkakati kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Kuishauri menejimenti ya Halmashauri juu ya masuala yanayohusiana na sera zinazohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
Kusimamia maendeleo ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano na utekelezaji wake kwa ajili ya Halmashauri.
Kutoa na kuratibu maswala yote ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano kwa menejimenti ya Halmashauri.
Kutathimini, kuboresha na kusimamia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na usimamizi wa mifumo mbalimbali iliyosimikwa kwenye Halmashauri.
Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo.
Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na namna ya kuthibiti.
Adam K. John
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA TEHAMA
HALMASHAURI YA WILAYA
KARAGWE
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.