DC LAIZER AONGOZA KIKAO CHA TATHIMINI YA MKATABA WA LISHE KWA NGAZI YA KATA KWA ROBO YA KWANZA JULAI-SEPTEMBA
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe: Julius Kalanga Laizer ameongoza Kikao cha Tathimini ya Utekelezaji wa Afua za Lishe ngazi ya Kata kwa robo ya kwanza kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ambapo amewasistiza Watendaji wa Kata kuendelea kusimamia upatikanaji wa chakula mashuleni kwenye maeneo yao na kuweka utaratibu rafiki kwa wazazi ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya Mhe: Laizer leo Novemba 14, 2025 amewasisitiza watendaji hao wa kata kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashamba darasa ya kulima mazao ambayo yatachangia kuongeza chakula Shuleni ili kusaidia watoto wenye mazingira magumu na wazazi ambao hawawezi kuchangia chakula shuleni.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi; Henrietta William amewahimiza Watendaji Kata kutumia majukwaa mbalimbali kuhamasisha Wananchi kutunza vyakula ili viwasadie wakati wa kiangazi na kuacha tabia ya kuuza mazao yote kwani kufanya hivyo ni kuwatesa watoto.

Akipitia kadi alama Afisa lishe Wilaya Bi; Asnat Thobias ameeleza kuwa katika Wilaya ya Karagwe tuna shule za msingi 157 na shule za Sekondari 29 na zote zinatoa huduma ya chakula Shuleni na kufikia asilimia 100 kama kadi alama ilivyonyesha.
Aidha, Bi; Asnat ameeleza mafanikio kwa kipindi cha robo ya Julai-Septemba kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto walinyonya maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo ambapo ni 8923 kati ya 9119 sawa na Asilimia (97.9%), Kupungua kwa idadi ya wajawzito wenye upungufu wa damu ambao ni 9 kati ya 5701 (0.2%)

Bi; Asnat alisisitiza Kuendelea kushirikiana kuhamasisha wazazi na walezi kwenye uchangiaji wa huduma ya chakula Shuleni kupitia majukwaa mbalimbali, Kuendelea kuhamasisha wanaume kujihusisha na masuala ya lishe ya familia ili maamuzi ya chakula iwe shirikishi kwa wote na Kuendelea na uelimishaji kwa akina Mama na wenza wao kuwahi klinik mapema mara anapojihisi wana ujauzito ili kupata huduma za Afya na uzazi mapema.

KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.