IDARA YA MAZINGIRA NA UDHIBITI TAKA NGUMU (ENVIRONMENT AND SOLID WASTE MANANGEMENT)
1.0: UTANGULIZI
Idara ya Mazingira na takangumu ni Idara mpya iliyoundwa mwaka 2013 kwa lengo la kuimarisha usafi wa mazingira na Hifadhi/utunzaji wa mazingira kuanzia ngazi ya Kaya,Kitongoji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa hadi Taifa. Kutokana na asili ya kazi za idara hii na mwongozo wa serikali, wataalam wa Idara hii wanapaswa kuwa na taalum ya Afya-mazingira kwa ajili ya kusimamia shughuli za usafi wa mazingira na wengine kuwa na taaluma ya Mazingira na Misitu kwa ajili ya kusimamia shughuli za hifadhi na utunzaji wa mazingira.
Hii ni kulingana pia, na matakwa ya kitaaluma na maelekezo ya sheria ya usimamizi wa mazingira Na. 20, ya 2004 na mpango kazi wa taifa wa hifadhi na usimamizi wa mazingira, 2013 – 18, likiwemo suala la udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, yaani, ardhi, hewa, kelele na uthibiti taka, pamoja na shughuli za kutathmini athari za mazingira. Uhundaji wa idara hii pia, utarahisisha uendeshaji, utendaji, utaratibu, mawasiliano na ushiriki wa wadau mbali mbali, wakiwemo wananchi, ambao ndiowalegwa wa huduma hizi za mazingira.
Wataalamu wa idara hii ni; wanasayansi wa mazingira (enviroment scientists) wahandishi mazingira ( environment engineers, sanitation engineers, public health engineers) na maafisa afya (environmental health scientists).
2.0:MAJUKUMU YA IDARA
2.1: HIFADHI YA MAZINGIRA
2.1.1 Utunzaji/Uhifadhi wa Mazingira na Bioanuai (Environmental Conservation and Biodiversity)
2.1.2 Udhibiti Uchafuzi wa Mazingira (ardhi, maji, hewa na sauti) (pollution contro: land, water,air and sound)
2.1.3 Tathmini ya Athari kwa Mazingira-TAM (Environmental Impact Assessment-EIA)
2.2.3. Uchambuaji Utupaji taka ngumu na Uendeshaji dampo la kisasa (Sorting And Sanitary Disposal Of Solid Waste And Dumpsite Management)
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.