Kitengo cha Ukaguzi wa ndani kimeanzishwa chini ya kifungu 45 (1) cha sheria ya fedha ya mamlaka ya Serikali za mitaa Na 13 ya mwaka 1982.Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Kamati ya Ukaguzi.
KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
MUUNDO, MAJUKUMU, WAJIBU NA UTOAJI HUDUMA
UTANGULIZI:
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani katika Halmashauri kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya fedha za Serikali za Mitaa Na. 9 (1982) Kf. 45 (1), Memoranda ya Fedha ya Serikali za Mitaa (2009) Kf. 13(1-2) na 14(1-10), sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 7 (2011) na marekebisho yake ya mwaka 2016 Kf. 48 (2). Sheria ya fedha za umma na.6 (2001) na marekebisho yake ya mwaka 2010, Mwongozo wa ukaguzi wa ndani wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 na mwongozo wa kimataifa wa ukaguzi wa ndani wa mwaka 2017 na mwongozo wa mchakato wa ukaguzi wa ndani wa mwaka 2016.
Kitengo kwa sasa kina jumla ya watumishi 2 ambao ni:-.
Ramadhani Omari Samizi - Mkaguzi wa Ndani
Ferdinand Bishashara - Mkaguzi wa Ndani
RASILIMALI ZA KITENGO
Kitengo kina rasilimali za kufanyia kazi ambazo ni komputa 2, printer 1, viti 2, meza 3, makabati 2, shelf 2 na gari 1 aina ya Toyota landcruiser pickup station wagon.
NYARAKA ZA OFISI
Kitengo cha ukaguzi kina nyaraka mbalimbali za ofisi kama vile jalada la ukaguzi wa ndani kwa ajili ya taarifa za ukaguzi mbalimbali, Memoranda ya Fedha ya mwaka 2009, Memoranda ya uhasibu ya mwaka 2009, Jalada la vielelezo, mpango wa ukaguzi wa mwaka.
SHUGHULI MUHIMU ZINAZOENDELEA
Katika kusimamia mpango kazi wa mwaka 2023/2024 shughuli muhimu zinazoendelea ni kuanza kazi za ukaguzi wa miradi ya maendeleo pamoja na kuwasilisha taarifa ya ukaguzi wa ndani robo ya pili.
Kulingana na muundo wake, Kitengo kinawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mtendaji katika kuwasilisha taarifa zake na kwa muundo uliopo sasa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina hadhi ya Idara kamili.
Sera ya kitengo ni kutoa huduma zake kwa wadau wake kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia miongozo, sheria, kanuni, maadili, uadilifu na kwa maarifa bila upendeleo bali kuweka mbele maslahi ya wadau wanaotegemea huduma zetu.
MAJUKUMU YA KITENGO
Majukumu ya Kitengo makubwa ni mawili ambayo ni kutoa ushauri wa ndani
(Internal consulting) na kutathimini mifumo ya udhibiti wa ndani (assurance
and appraisal) juu ya raslimali fedha na nyinginezo katika Halmashauri. Lakini
kufikia majukumu hayo mawili kazi hizo hufanyika.
Kuandaa mpango kazi wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa mwaka kuandaa mipango ya Ukaguzi.
Kutoa ushauri juu ya uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya ndani.
Kutoa ushauri juu ya kubaini maeneo yenye vihatarishi vikubwa katika utendaji kazi wa kufikia malengo ya Idara, Kitengo au Halmashauri nzima.
Kutoa taarifa za matokeo ya ukaguzi kwenye menejimenti ili hatua za kuimarisha ufanisi zichukuliwe.
Kufanya ukaguzi maalum kuhusu tuhuma zinazotolewa au zilizopo.
Kuwezesha kamati ya Ukaguzi kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kufuatilia na kutoa ushauri juu ya menejimenti kuhakikisha hoja za Mkaguzi wa nje zinajibiwa kwa wakati.
Kuandaa maeneo yenye kuhitaji kukaguliwa kwa kuzingatia umuhimu na athari zake kwa Halmashauri.
Kuandaa mipango ya ukaguzi wa miradi kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Kushughulikia kazi zingine zitakazo agizwa na Mkurugenzi Mtendaji bila kuathiri nafasi ya majukumu yake katika utendaji kazi wake.
WADAU WA KITENGO
Kutokana na umuhimu wake kitengo kina wadau mbalimbali wa ndani na nje ya taasisi
yetu ambao ni:-
Serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa, Wizara ya Fedha, Afya, Kilito, Maji, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu).
Menejimenti (Baraza la Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo).
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Wadi (Wazabuni na Wakandarasi)
Asasi zisizo za Kiserikali.
Wananchi wa Wilaya ya Karagwe.
HALI YA UTOAJI HUDUMA
Kitengo kinafanya kazi katika kupitia na kutoa taarifa kuhusu usimamizi wa mapato na matumizi, raslimali mali na watu, utawala bora, ushirikishwaji na uwazi katika manunuzi ya umma.
Mawanda ya utendaji kazi wa kitengo ni mpana na katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi uwezeshwaji wa dhati kutoka kwenye menejimenti hauna budi kufanyika.
FURSA ZILIZOPO:
Kitengo kina fursa mbalimbali ambazo inazitumia kuongeza ufanisi na ubora wa huduma kazi na kwa Halmashauri kwa ujumla. Baadhi yake ni kama ifuatavyo:-
Kitengo cha Ukaguzi wa ndani kilipata gari la kufuatilia miradi na taasisi ngazi za chini.
Kuwepo kwa mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za fedha.
Idara nyingi kuwa na vitendea kazi vya kompyuta ambazo zinarahisisha upatikanaji na utunzaji wa taarifa kwa wakati.
Ushirikiano wa dhati toka kwa baadhi ya wakuu wa idara kuwezesha kitengo kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Watumishi kuruhusiwa kuhudhuria mafunzo na semina kwa ajili ya kuboresha ufahamu na taaluma.
Ikama ya kitengo cha Ukaguzi wa ndani kutofikiwa
HITIMISHO:
Tunapenda kutoa shukrani kwa wadau wetu mbalimbali kwa ushirikiano mkubwa tunaoupata na kutuwezesha kufanya kazi zetu. Baadhi ya wadau tunaofanya nao kazi kwa ukaribu ni Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara, Baraza la Madiwani, Kamati zote za Kudumu, Kamati ya Ukaguzi, Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali Mkazi Kagera na Ofisi ya mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.