• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
KARAGWE DISTRICT COUNCIL
KARAGWE DISTRICT COUNCIL

United Republic of Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na dira
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu
        • Sekondari
        • Msingi
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Mazingira na Taka ngumu
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Ufugaji na Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Elimu, Afya na Maji
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Inayokuja
    • Iliyotekelezwa
    • Inayoendelea
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Taarifa
    • Sheria
    • Mpango mkakati
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

Historia

CHIMBUKO/ASILI YA KARAGWE NA WATU WAKE (WANYAMBO)

Kutokana na simulizi za wazee na watafiti mbalimbali kama vile Katoke (1975; 162) jina ‘Karagwe’ jina linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala ( Omukama ) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba mtawala huyo alijulikana kwa jina la ‘Nono ya Malija’ kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya "Karagwe ka Nono "inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara. Inasemekana kwamba Nono aliondolewa kwa ujanja bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la historia ya jina Karagwe.

MIPAKA YA WILAYA.

Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya saba (7) za Mkoa wa Kagera. Wilaya ya Karagwe inapakana na Wilaya ya Kyerwa upande wa Kaskazini, nchi ya Rwanda upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba upande wa Mashariki.

JIOGRAFIA YA WILAYA.

Wilaya ipo kilomita 105 kutoka Manispaa ya Bukoba –Makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Wilaya inapatikana kati ya nyuzi 1o na 2o, 20' Kusini Latitudo 30o hadi 38,30 Mashariki Longitudo. Mwinuko wa ardhi kutoka usawa wa bahari ni mita 1,500 hadi mita 1,800. Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa degree 26oC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa mm 1,040 hadi 1,200 kwa mwaka, kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na mwezi Mei.

ENEO LA WILAYA.

Wilaya ya Karagwe ina eneo la kilomita za mraba 4,500 kati ya hizo kilomita za mraba 4,342 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 158 ni eneo la maji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 153,540 na eneo linalolimwa ni Hekta 82,808.5 sawa na asilimia 53.9.

UTAWALA.

Kwa upande wa maeneo ya utawala, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ina Tarafa tano (5) ambazo ni Bugene, Nyakakika, Nyaishozi, Nyabiyonza na Kituntu. Pia wilaya ina kata 23, vijiji 77 na vitongoji 612 ambapo kati ya vitongoji hivyo 612, vitongoji 20 vipo katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga na vinaitwa vitongoji kwa sababu bado mamlaka hiyo ya mji mdogo haijawa mamlaka kamili ili vitongoji hivyo viitwe mitaa. Halmashauri ya wilaya ina waheshimiwa madiwani 32 ambapo kati yao 23 ni wa kuchaguliwa kutoka katika kata za Halmashauri ya Wilaya, 8 ni wa viti maalum na mbunge wa Jimbo 1.

IDADI YA WATU.

Kulingana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Karagwe ilikuwa na jumla ya watu wapato 332, 020. Kati ya hao 163,864 (wanaume) na 168,156 (wanawake), ambapo ongezeko la watu ni asilimia 2.9 kwa mwaka.

Maoteo ya watu kwa mwaka 2015 ni kuwa Wilaya ilikuwa na watu 351,555. Kati ya hao, wanawake ni 178,050 na wanaume ni 173,505. Aidha idadi ya kaya nayo imeongezeka toka kaya 72,836 mwaka 2012 hadi kaya 76,425 mwaka 2015.

 SHUGHULI ZA KIUCHUMI:

1. KILIMO, USHIRIKA NA UMWAGILIAJI:

Kilimo ni mojawapo ya shughuli za kiuchumi inayochangia wastani wa asilimia 70 ya pato la Halmashauri. Kaya zinazoshiriki katika shughuli za kilimo ni 61,351 kati ya kaya zote 76,425 za wilaya ya Karagwe. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 153,540 kati ya hekta 4,500,000 ya eneo lote la wilaya. Eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 4,500 Pia Wilaya inashirikiana na wadau mbalimbali waliopo wilayani katika kuendeleza sekta ya kilimo. Baadhi ya wadau hao ni ELCT, Karagwe Agribusiness, MAVUNO, CHEMA, WORLD VISION, MATUNDA MEMA, BISHESHE WINE, KARAGWE ESTATE LTD, RADIO KARAGWE, RADIO FADECO, LUKALE WINE, KDCU, Matunda MEMA, KADERES NA OLAM.

Aidha zipo SACCOS 31 zenye jumla ya wanachama 46,319 na Chama 1 kikuu cha Ushirika (KDCU) kinachojishughulisha na ununuzi wa mazao ya wakulima. Wilaya imeanzisha na kujenga mradi mmoja mkubwa wa Umwagiliaji (Mwisa Irrigation Scheme) wenye ukubwa wa Hekta 120. Uhamasishaji wa wananchi kulima mpunga na mbogamboga unaendelea. Mradi huu utaongeza kipato cha mkulima wa Karagwe na kupunguza umaskini.

2. UFUGAJI NA UVUVI:

Wilaya ya Karagwe ina hekta 140,000 zinazofaa na hutumika kwa shughuli za ufugaji. Sekta hii uchangia kwa zaidi ya 10% katika ajira ya wananchi na pato la kaya. Mifugo ambayo hufugwa ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na sungura.

Shughuli za Uvuvi ufanyika katika maziwa madogo ya Burigi, Rwakajunju, Kamakala na mto Kagera. Wilaya inayo mabwawa ya kuchimbwa 67 kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Uzalishaji wa samaki ni wastani wa kilo 33,000 kwa mwaka. Aina za samaki wanaozalishwa kwa wingi ni sato/ngege, kambale mamba, kambale mumi, furu, ningu, soga na domodomo.

3. VIWANDA NA BIASHARA:

 Mji wa Kayanga na Omurushaka pamoja na miji midogo ya Kihanga, Nyakaiga, Rwambaizi, Nyaishozi, Chanyamisa, Nyabiyonza, Nyakabanga na Ihembe ni kati ya miji inayokua kibiashara na yenye mwingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii.  Maeneo haya yanaendelea kuwekeza katika viwanda vya biashara kama vile viwanda vya kukoboa Kahawa, viwanda vya kusindika maziwa, asali, kusaga na kukoboa nafaka. Shughuli za uzalishaji zinaendelea kuimarika na kuongeza uzalishaji, kupanua ajira, kukuza biashara ya uuzaji na ununuzi wa mazao tarajiwa na hivyo kuongeza kipato na kukuza uchumi, kuboresha maisha ya jamii, kupunguza umaskini wa kipato na hivyo kuchochea kasi ya kuondoa umaskini.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMI 10 October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA DEREVA II NA WAANDISHI WAENDESHA OFISI II September 30, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WASAIDIZI KUMBUKUMBU DARAJA LA II NA MTENDAJI WA KIJIJI WA III October 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI February 21, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAKETI KUJADILI UTEKELEZAJI WA AFUA ZA LISHE, KIPINDI CHA ROBO YA TATU 2024/2025.

    April 22, 2025
  • KUELEKEA MSIMU WA KAHAWA 2025/2026: MAAFISA UGANI KARAGWE DC WAPEWA MAFUNZO ILI KUWASAIDIA WANANCHI KUONGEZA THAMANI YA ZAO HILO.

    April 11, 2025
  • WALENGWA WA TASAF KARAGWE DC WANUFAIKA NA VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA KIFEDHA WALIZOANZISHA.

    March 17, 2025
  • DC LAIZER AWATAKA WANAWAKE WA KARAGWE KUJIIMARISHA KIUCHUMI.

    March 08, 2025
  • Angalia zote

Video

SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 KARAGWE TUMEJIPANGA
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • History
  • Dira na Dhamira
  • Fomu za mbalimbali
  • NEEMA INAKUJA KWA WAKULIMA
  • FEDHA ZILIZOPOKELEWA KWA AJILI YA MFUKO WA JIMBO

Viunganishi vihusishi

  • NECTA
  • UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAIFA
  • TAMISEMI
  • FFARS
  • SALARY SLIP

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    KARAGWE KAGERA TANZANIA

    Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE

    Simu: 028-2227148

    Simu ya mkononi: 028-2227148

    Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani elekezi
    • Huduma

Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.