IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII
UTANGULIZI
1.0. UTANGULIZI
Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Divisheni za Halmashauri kulingana na mwongozo.Divisheni ina Sehemu mbili kama ilivyoainishwa katika mwongozo wa majukumu ya Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ambayo ni:-
1.Uratibu wa masuala Mtambuka
2.Uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi vya kijamii
2.0. WATUMISHI WA DIVISHENI YA MAENDELEO YA JAMII
Diveshini ya Maendeleo ya Jamii ina watumishi kumi na Sita (16) kati ya hao, watumishi saba (7) wako ngazi ya Makao makuu na watumishi waliobakia Nane (8) wapo katika ngazi ya Kata. Aidha, Halmashauri ina Kata 23, na Vijiji 77 hivyo tuna upungufu wa watumishi 93 (ngazi ya kata watumishi 16 na ngazi ya kijiji watumishi 77). Mtumishi mmoja ambaye ni mlezi wa Watoto anahudumia katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga
3.0 MIRADI YA MAENDELEO YA JAMII/SHUGHULI ZA IDARA
Divisheni ya Maendeleo ya Jamii pamoja na utekelezaji wa miradi mingine imetekeleza shughuli zifuatazo:-
Ufuatiliaji wa Vikundi juu ya urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 inayodaiwa na ushauri wa uanzishaji wa miradi ya vikundi yenye uendelevu katika kata zote 23 ambapo Sh. 130,177,800 zimerejeshwa.
Ufuatiliaji wa marejesho ya vikundi vilivyokopeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana toka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) kiasi cha Sh. 12,418,000 zimerejeshwa.
Kutoa Elimu ya Malezi, Makuzi ya Awali ya Mtoto na Ulinzi na Usalama wa Mtoto kupitia Redio Karagwe vipindi 3 na kupitia mikutano ya hadhara.
Kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kupitia Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika kata 23 wilayani, ambapo jumla ya watu 4322 walifikiwa. Kauli Mbiu “Wekeza, kupinga Ukatili wa Kijinsia.”
Ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) na kufanya kikao cha pamoja wakati wa maandalizi ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
Kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kuchangia miradi ya Maendeleo kwa kushirikiana na Shirika la CBIDO katika kata za Chonyonyo na Kamagambo.
4.0 UKIMWI
Mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI:
Jumla ya Kondomu 63,000 zimesambazwa kwenye maeneo yenye mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU (Nyumba za kulala wageni, stendi, Baa na vigata) na elimu ya kujikinga na maambukizi mapya kwa vijana.
Kutoa elimu juu ya madhara ya VVU/UKIMWI kupitia redio Fadeko kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani tarehe 01/12/2023, ambapo maadhimisho yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari kata Bugene. Kauli mbiu: “Jamii Iongoze, kutokomeza UKIMWI”.
Kufanya Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani tarehe 8.03.2024 yenye lengo la kutoa elimu kwa wanawake kwa maendeleo na ustawi wa Taifa, Kulifanyika kongamano na kutoa msaada kwa wahitaji na kuchangia jitihada za Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa aliyofanya kwa kujenga miundombinu ya madarasa hivyo kuweza kuchangia madawati 15 katika shule ya Msingi ya Nyakahanga yenye thamani ya Tshs 1,275,000/=
5.1 SHUGHULI ZA TASAF
i). Kwa kipindi cha mwaka 2023 jumla ya Tsh. 344,571,755 Taslim zilipokelewa kwa ajili ya malipo kwa walengwa 4,175 na Tsh 606,530,831zilipokelewa kwa njia ya simu na kupitia Benki kwa walengwa 6,775. Aidha, Tsh 6,712,805 zililipwa kwa ajili ya kutolea katika simu na Gharama za kutolea Benki Tsh 20,865,600 (miamala). Hivyo jumla ya fedha zilizopokelewa kwa ajili ya malipo ya walengwa kuwa Tsh 978,680,991 kwa ajili ya dirisha la Julai - Agosti na Septemba-Oktoba, 2023.
ii) Tathmini ya hali ya maendeleo ya walengwa kwa vijiji 57 vilivyoingia TASAF mwaka 2015 kwa ajili ya maandalizi ya kuziondoa kaya zilizoimarika kiuchumi. Aidha, utaratibu unaoendelea kwa sasa ni kuchambua na kuhuisha taarifa katika mfumo kwa ajili ya kupata taarifa ya mwisho ya malipo ya walengwa kwa kipindi hiki.
iii) Uhamasishaji wa Walengwa wa TASAF kuanzisha vikundi vya Huduma ndogo za kifedha kwa lengo la kujenga uwezo wa kujitegemea pia kuanzisha shughuli za kiuchumi kwa kuanzisha miradi na kuweka akiba jumla ya vikundi 452 vimeundwa na mpaka sasa Jumla ya vikundi 205 vimesajili na taratibu za usajili wa vikundi hivi unaendelea kwa mujibu wa taratibu za sheria ya huduma ndogo za kifedha 2018. Aidha vikundi hivi vinatokana na vijiji 57 vya mwanzo wa utekelezaji wa mradi ikiwa bado zoezi hili litafanyika katika vijiji vipya 20 vilivyobaki.
6.0. UWEZESHAJI KIUCHUMI (UTOAJI WA MIKOPO)
Divisheni ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikiratibu na kusimamia Mfuko wa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kupitia mapato ya ndani ya 10% kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kuanzia mwaka 2014/2015 hadi 2022/2023, Jumla 2,605,370,302 zimekopeshwa na kiasi cha Shilingi 2,277,596,747 zimerejeshwa na kiasi cha Shilingi 328,073,573.00 ni deni la ndani na nje ya mkataba.Kama inavyooneshwa kwenye jedwali na.1
JEDWALI NA 1: HALI YA UTOAJI WA MIKOPO NA MAREJESHO
NA
|
MWAKA
|
MKOPO BILA RIBA
|
MKOPO NA RIBA
|
MAREJESHO
|
DENI
|
1
|
2014/2015
|
64,500,000.00
|
69,615,000.00
|
67,968,500.00
|
1,646,500.00
|
2
|
2015/2016
|
130,188,000.00
|
144,494,320.00
|
103,546,343.00
|
40,947,977.00
|
3
|
2016/2017
|
196,000,000.00
|
209,930,000.00
|
195,354,604.00
|
14,575,396.00
|
4
|
2017/2018
|
103,300,000.00
|
110,531,000.00
|
102,053,000.00
|
8,478,000.00
|
5
|
2018/2019
|
311,000,000.00
|
311,000,000.00
|
288,232,100.00
|
22,767,900.00
|
6
|
2019/2020
|
388,000,000.00
|
388,000,000.00
|
366,785,500.00
|
21,214,500.00
|
7
|
2020/2021
|
432,000,000.00
|
432,000,000.00
|
411,801,500.00
|
20,498,500.00
|
8
|
2021/2022
|
524,300,000.00
|
524,300,000.00
|
457,001,100.00
|
67,298,900.00
|
9
|
2022/2023
|
415,500,000.00
|
415,500,000.00
|
284,854,100.00
|
130,645,900.00
|
|
JUMLA
|
2,564,788,000.00
|
2,605,370,320.00
|
2,277,596,747
|
328,073,573.00
|
Aidha, kwa Mwaka 2023/2024 fedha za mikopo kwa Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu hazijakopeshwa kutokana na Agizo la serikali la kusitisha utoaji wa mikopo, Halmashauri mpaka sasa imetenga na kukusanya kiasi cha Tsh 1,103,301,699.29 (kiasi cha Tsh 852,624,967.06 ni fedha za marejesho na kiasi cha Tsh 250,676,732.23 ni fedha za Mapato ya ndani 10%) kwenye akaunti ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni fedha za marejesho na asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Kwa Kushirikiana na Benki ya CRDB kupitia fursa ya kuwezesha wanawake mitaji (IMBEJU) vikundi 3 vya wanawake vyenye wanakikundi 10 vimepatiwa mkopo wa Tshs 33,000,000.Pia uhamasishaji wa vikundi kunufaika na fursa hii unaendelea.
6.1 Mkakati wa marejesho
Aidha, Usajili wa vikundi 283 vya huduma ndogo za kifedha kwa mujibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwka 2018 na Utambuzi wa vikundi 2,021 vya kijamii na Kiuchumi kutoka kata za Halmashauri vimetambuliwa
7.0. MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YALIYOPO KATIKA HALMASHAURI
Haimashauri ina jumla ya Mashirika 22. Mashirika yote yanajishughulisha na shughuli za kijamii/kimaendeleo na kusaidia makundi maalum.Mashirika hayo ni kama ifuatavyo:-
1. KCBRP
2. MAVUNO 3. WORLD VISION 4. CBIDO 5. TOSO 6. KARADEA 7. HUMULIZA 8. SFT 9. KEQI 10. APROFI 11. SAWAKA 12. KESUDE 13. COEHI 14. UWASHEKA 15. PCC 16. KARUDECA 17. HEMDT 18. KARUPOA 19. TAWILO 20. MDH 21. KARUPOA 22. MKUTA FOUNDATION |
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.