Ufugaji nyuki ni kati ya kazi za kiuchumi zinazofanywa na watu wa Wilaya ya Karagwe. Kazi ya ufugaji Nyuki hufanywa na watu binafsi, vikundi vya kijamii (CBO’s), taasisi (NGO,s) na taasisi za umma kama vile mashule. Mpaka sasa kuna idadi ya wafugaji nyuki na vikundi 258, idadi ya mizinga ya kisasa 3,551, mizinga ya kienyeji 5,592, jumla ya mizinga yote 7,143, kiasi cha asali kinachotegemewa kuvunwa ni Kg 91,430, na kiasi cha nta ni Kg 18,286U
wekezaji katika Sekta ya Nyuki
Changamoto zinazoikabili Sekta ya Ufugaji wa Nyuki
Mkakati wa kuendeleza sekta ya ufugaji wa nyuki.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA SEKTA YA UFUGAJI NYUKI KWA MWAKA 2016/2017
Madhumuni ya Ufugaji Nyuki
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria ya Ufugaji Nyuki Namba 15 ya mwaka 2002 na Kanuni zake za mwaka 2005, ufugaji nyuki una malengo makuu matatu ambayo ni:
Ili kuweza kutekeleza malengo tajwa hapo juu, Kitengo cha Ufugaji Nyuki kimefanya yafuatayo kwa mwaka 2016/2017.
A: Kazi zilizofanyika kwa kipindi tajwa ni kama ifuatavyo
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi waliofika ofisini: Jumla ya wanachi 28 walifika ofisini kwa vipidi tofauti kuomba ushauri wa njia bora za ufugaji nyuki. Ushauri uliotelewa ni pamoja na njia bora za utengenezaji, uambikaji na utundikaji wa mizinga, jinsi ya kutengeneza mizinga ya kisasa (modern bee hives), jinsi ya kuboresha mizinga ya asili ili kulinda ubora wa mazao yanayovunwa, habari ya masoko kwa mazao ya nyuki na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Kuendesha mafunzo ya ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira kwa njia ya redio: Jumla ya vipindi 43 vya utunzaji wa mazingira kupitia upandaji wa miti, utunzaji wa vyanzo vya maji na ufugaji nyuki kupitia Redio FADECO vilienda hewani. Vipindi hivi vilirushwa kila siku ya jumatatu ya wiki kuanzia saa 3.00 – 4.00 asubuhi. Vipindi hivi havilipiwi na Halmashauri gharama yoyote bali ni mchango wa redio katika kuielimisha jamii na kuongeza hamasa ya ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.
Kuhusu ufugaji wa nyuki, vipindi hivi viliielimisha jamii juu ya mada zifuatazo:
Mafunzo haya yalikuwa na madhumini yafuatayo kwa jamii:
Kutembelea wafugaji nyuki vijijini na kuwaelimisha juu ya ufugaji bora: Vikundi vya wafugaji nyuki na wafugaji binafsi waliko maeneo mbalimbali ya Karagwe walitembelewa kwa lengo la kuwaelemisha na kuwashauri juu ya upunguzaji wa changamoto walizonazo.
Maeneo ya ufugaji nyuki Karagwe
Nyuki wanafugwa kwenye kata zote 23 za wilaya ya Karagwe lakini maeneo yanayofuga zaidi nyuki ni pamoja na;
Kata ya Bweranyange kwenye vijiji vya Muguruka na Chamchuzi
Kata ya Nyakasimbi kwenye vijiji vya Muungano na Chanyamisa
Kata ya Rugu kwenye vijiji vya Ruhita, Misha na Rugu
Kata ya Kihanga kwenye vijiji vya Kihanga, Katanda na Mulamba
Kata ya chanika kwenye vijiji vya Mchuba, Chanika na Runyaga na Ruzinga
Kata ya Nyakahanga kwenye vijiji vya Nyakahanga, Rwandalo, Omurusimbi na Bisheshe
Kata ya Rugera kwenye vijiji vya Rugera, Omukakajiji na Nyarugando
Kata ya Nyaishozi kwenye vijiji vya Rukale na Nyakayanja na
Kata ya Igurwa kwenye kijiji cha Kigarama.
Maeneo tajwa hapo huu yametembelewa zaidi kutokana na hatuwa waliokwisha fikia kwenye swala zima la ufugaji nyuki, ingawa pia na maeneo mengine ya Halmashauri yalitembelewa ili kuongeza hamasa ya ufugaji yuki.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
||||||
|
|
|
|
|
|
|||
|
||||||||
|
||||||||
|
|
Ukusanyaji wa takwimu: Takwimu zilizokusanywa hadi mwishoni mwa mwaka 2016/2017 ni kama ifuatavyo kwenye jedwari hapa chini:
Idadi ya mizinga yenye nyuki |
Idadi ya mizinga isiyo na nyuki |
Jumla ya mizinga yote |
|||
mizinga ya kisasa
|
mizinga ya asili
|
mizinga ya kisasa
|
mizinga ya asili
|
mizinga ya kisasa
|
mizinga ya asili
|
1755 |
5981 |
882 |
2685 |
2637 |
8666 |
Takwimu hizo zinaonyesha kuwa kuna jumla ya makundi ya nyuki 7,736 yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha Kilogramu za asali 77,360 (kwa wastani wa kila mzinga Kg 10 za asali) na Kg 15,472 (kwa wastani wa kila mzinga Kg 2 za nta). Changamoto kubwa iliyopo ni kudhibiti njia za usafirishaji wa mazao haya hasa kwenda nje ya nchi na ukweli wa wafugaji kueleza kiasi hasa wanachovuna. Hili linasababisha kutopata takwimu za kutosha za mazao yanayovunmwa na kuuzwa. Kwa takwimu za mizinga na makundi ya nyuki kwa kila kata angalia kiambatanisho A.
Soko la mazao ya nyuki:
Kwa sasa wanunuzi wakuu wa mazao ya nyuki Karagwe ni CHEMA- Omurushaka na shirika la OLAM. Wanunuzi wengine ni warejareja kwenye masoko ya Kayanga, Omurushaka, Chanyamisa na miji mingine midogo midogo iliyoko Karagwe. Kutokana na kuhitajika kwa asali hasa kwa ajili ya chakula na dawa hakuna mfugaji nyuki anayezalisha asali akakosa soko. Hii inaonyesha kuwa soko la ndani bado lipo na wafugaji tunawahimiza wazalishe zaidi ili tukuze soko la ndani na pia la nje ya Wilaya.
Makampuni makubwa ya ununuzi wa asali yaliyoko kwenye mikoa mingine hasa miko ya kati yamekuwa na ugumu wa kuja kununua asali kwenye wilaya za huku pembezoni kutokana na uzalisha mdogo wa mazao ya nyuki uliopo na umbali pia. Nawashauri vikundi vya nyuki na wafugaji wetu kununua vigungashio na kuuza asali zao moja kwa moja kwa mlaji wa ndani na nje ya wilaya badara ya kusubiri makampuni kutoka nje ya wilaya.
Taasisi za MAVUNO na FADECO nazo ziko kwenye maandalizi ya kuanza kununua, kufungasha na kuuza mazao ya nyuki.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||
|
|
|
|||||
|
|
||||||
|
|||||||
|
|||||||
|
|||||||
|
|
|
Ushirikiano na taasisi nyingine: Kitengo kimeendelea kushirikiana na taasisi nyingine katika kuendeleza ufugaji wa nyuki kwa lengo la kupunguza umaskini na kutunza mazingira. Taasisi tunazofanya kazi nazo ni pamoja na CHEMA, ELCT, MAVUNO, World Vision, Redio FADECO na OLAM.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||
|
|||||
|
|
B: Changamoto
Uharibifu wa mazingira: kazi za binadamu hasa uchomaji moto ovyo, ukataji miti ovyo, matumizi ya dawa za kilimo (herbicides), ufugaji wa mifugo hasa matumizi ya dawa za kuua kupe (acaricides), na kazi nyinginezo zimechangia katika kupunguza makundi ya nyuki.
Ukosefu wa mvua za uhakika kwa kipindi kirefu: kutokana na tatizo la ukame lililoikumba Wilaya ya Karagwe na maeneo mengine hasa kwenye nusu ya kwanza ya mwaka 2016/017, makundi ya nyuki yalikuwa haba na kuchangia mizinga mingi kukosa makundi ya nyuki kwa mda mrefu. Hili lilisababisha baadhi ya mizinga kuanza kuharibika na baadhi ya vikundi kuanza kusambaratika kutokana na kukata tamaa.
Mwamuko ndogo wa jamii: bado jamii kubwa haina mwamuko wa kutosha katika sekta hii kutokana na asili ya watu wa Karagwe ukilinganisha na makabila mengine hapa nchini. Hili limesababisha ukuaji mdogo wa sekta hii kwa wilaya ya Karagwe pamoja na juhudi zinazoendelea kufanyika za uhamasishaji zinazofanywa na Halmashauri na mashirika binafsi.
Matatizo ya soko huria: Kila mara imekuwa ni vigumu kupata takwimu za kutosha hasa za mazao ya nyuki kutokana na wafugaji wengi kuuza mazao ya nyuki kwa wanunuzi wanaotoka ndani na nje ya nchi bila kupita ofisini kwetu.
C: Mkakati wa kuendeleza sekta ya ufugaji wa nyuki na kupunguza changamoto
Mkakati wa Kitengo cha Nyuki ni pamoja na;
D: Taarifa ya mizinga 1000 ya mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana:
Jumla ya vikundi 28 vya wanawake na vijana vilipewa mkopo wa mizinga 1000 ya kisasa (top Bar Hives). Hadi mwishoni mwa mwaka 2016/017 mizinga 563 sawa na asilimia 56.3 ya mizinga yote imepata makundi ya nyuki na mizinga na 437 sawa na asilimia 43.7 haijapata makundi ya nyuki. Vikundi vingine zaidi ya nusu ya mizinga waliopewa imepata makundi ya nyuki na vingine ni chini ya nusu. Orodha ya vikundi na mizinga walionayo imeambatanishwa kama ‘kiambatanisho B’.
Sababu za matokeo tajwa hapo juu:
Thamani ya mradi:
Jumla ya Tsh. 62,188,000/= zilitumika kununua mizinga 1,000 ambapo bei ya kila mzinga ilikuwa Tsh. 62,118/=. Riba ya asilimia 14 ilitakiwa kulipwa na mtaji (principal) na hivo jumla ya Tsh. 70,894,320/= zinatakiwa kulipwa na mradi (wanavikundi). Mkopo huu unatakiwa kuanza kulipwa baada ya mwaka mmoja ambao umeisha june 2016 na ni matumaini kuwa baadhi ya vikundi wataanza kurejesha.
Naomba kuwasilisha.
Rajabu Khasimu
K.NY. MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
KARAGWE.
Kiambatanisho B Taarifa ya maendeleo ya Vikundi vya vijana na wanawake vilivyokopeshwa mizinga hadi mwezi Juni 2017 |
|
||||||
Na.
|
Jina la kikundi
|
Namba ya usajiri
|
Kata
|
Kijiji
|
Jumla ya mizinga
|
mizinga yenye nyuki
|
mizinga isiyo na nyuki
|
1
|
UKIWACHO
|
KDC/CD/CBO/033
|
Chonyonyo
|
chonyonyo
|
25 |
18 |
7 |
2
|
Twejune
|
KDC/CD/CBO/082
|
Nyakahanga
|
Nyakahanga
|
25 |
11 |
14 |
3
|
Nguvu Kazi
|
KDC/CD/CBO/120
|
Rugera
|
Nyarugando
|
50 |
38 |
12 |
4
|
Bora Imani
|
KDC/CD/CBO/173
|
Igurwa
|
Kigarama
|
50 |
27 |
23 |
5
|
Kimiza Pamoja Group
|
KDC/CD/CBO/154
|
Kihanga
|
Kishoju
|
50 |
36 |
14 |
6
|
UMAM
|
Reg: 233215
|
Chanika
|
Mchuba
|
50 |
47 |
3 |
7
|
KIWAWAVIKA
|
KDC/CD/CBO/150
|
Kituntu
|
Katwe
|
50 |
24 |
26 |
8
|
Umoja Rugera
|
KDC/CD/CBO/143
|
Rugera
|
Rugera
|
50 |
4 |
46 |
9
|
KIWAKAKA
|
KDC/CD/CBO/230
|
Kihanga
|
katanda
|
50 |
9 |
41 |
10
|
Umoja ni mali
|
KDC/CD/CBO/428
|
Igurwa
|
Bwera
|
50 |
30 |
20 |
11
|
Juhudi group
|
KDC/CD/CBO/420
|
Chonyonyo
|
Chonyonyo
|
50 |
40 |
10 |
12
|
Faraja
|
KDC/CD/CBO/136
|
Nyakahanga
|
Rwandalo
|
25 |
20 |
5 |
13
|
Tuinuane
|
KDC/CD/CBO/128
|
Rugu
|
Rugu
|
25 |
16 |
9 |
14
|
Tweyememu
|
KDC/CD/CBO/275
|
Kihanga
|
Nyarwele
|
25 |
11 |
14 |
15
|
Mavuno
|
KDC/CD/CBO/043
|
Nyakasimbi
|
Muungano
|
25 |
21 |
4 |
16
|
Tuyatunze mazingira
|
KDC/CD/CBO/696
|
Ihanda
|
Ihanda
|
25 |
21 |
4 |
17
|
Tuinuane
|
KDC/CD/CBO/478
|
Bweranyange
|
Muguluka
|
25 |
22 |
3 |
18
|
Wapendanao
|
KDC/CD/CBO/190
|
Ihembe
|
Ihembe
|
25 |
23 |
2 |
19
|
Wanambingu
|
KDC/CD/CBO/705
|
Kayanga
|
Kayanga
|
25 |
6 |
19 |
20
|
Tuinuane Rwambaizi
|
KDC/CD/CBO/189
|
Kanoni
|
Rwambaizi
|
50 |
13 |
37 |
21
|
Tupendane Kanoni
|
KDC/CD/CBO/479
|
Kanoni
|
Kanoni
|
50 |
8 |
42 |
22
|
Rugabo ELCT group
|
KDC/CD/CBO/510
|
Rugu
|
Misha
|
25 |
14 |
11 |
23
|
Furaha group
|
KDC/CD/CBO/288
|
Kituntu
|
Kinyinya
|
25 |
23 |
2 |
24
|
Mchaka Mchaka
|
KDC/CD/CBO/703
|
Nyaishozi
|
Nyaishozi
|
25 |
17 |
8 |
25
|
Umoja Wajasiliamali
|
KDC/CD/CBO/608
|
Kayanga
|
Kayanga
|
25 |
5 |
20 |
26
|
Muungano
|
KDC/CD/CBO/795
|
Kanoni
|
Rwambaizi
|
25 |
21 |
4 |
27
|
Hosiana A. group
|
KDC/CD/CBO/850
|
Ndama
|
Nyabwegira
|
25 |
8 |
17 |
28
|
Mshikamano Group
|
KDC/CD/CBO/856
|
Nyaishozi
|
Nyakayanja
|
50 |
30 |
20 |
|
jumla ya mizinga yote
|
|
|
|
1000 |
563 |
437 |
|
Kiambatanisho A Takwimu za mizinga ya nyuki kwa kila kata |
|
|
|
|||||
S/NO:
|
Jina la kata |
Idadi ya mizinga yenye nyuki |
Idadi ya mizinga isiyo na nyuki |
Jumla ya mizinga yote |
|||||
|
mizinga ya kisasa
|
mizinga ya asili
|
mizinga ya kisasa
|
mizinga ya asili
|
mizinga ya kisasa
|
mizinga ya asili
|
|||
1 |
Nyaishozi
|
133 |
123 |
42 |
82 |
175 |
205 |
||
2 |
Ihembe
|
54 |
198 |
36 |
132 |
90 |
330 |
||
3 |
Nyakasimbi
|
39 |
228 |
12 |
93 |
51 |
321 |
||
4 |
Rugu
|
52 |
268 |
79 |
370 |
131 |
638 |
||
5 |
Nyakabanga
|
43 |
52 |
14 |
36 |
57 |
88 |
||
6 |
Nyakakika
|
0 |
22 |
0 |
8 |
0 |
30 |
||
7 |
Bweranyange
|
68 |
2,796 |
57 |
789 |
125 |
3585 |
||
8 |
Kibondo
|
5 |
26 |
0 |
28 |
5 |
54 |
||
9 |
Nyabiyonza
|
7 |
303 |
3 |
239 |
10 |
542 |
||
10 |
Kiruruma
|
81 |
70 |
26 |
22 |
107 |
92 |
||
11 |
Kamagambo
|
90 |
136 |
20 |
30 |
110 |
166 |
||
12 |
Chonyonyo
|
74 |
159 |
58 |
51 |
132 |
210 |
||
13 |
Ihanda
|
123 |
54 |
24 |
11 |
147 |
65 |
||
14 |
Nyakahanga
|
89 |
272 |
56 |
166 |
145 |
438 |
||
15 |
Bugene
|
21 |
55 |
3 |
13 |
24 |
68 |
||
16 |
Kayanga
|
96 |
59 |
47 |
14 |
143 |
73 |
||
17 |
Rugera
|
41 |
338 |
62 |
69 |
103 |
407 |
||
18 |
Kihanga
|
352 |
318 |
137 |
112 |
489 |
430 |
||
19 |
Kituntu
|
52 |
71 |
35 |
22 |
87 |
93 |
||
20 |
Ndama
|
23 |
10 |
15 |
78 |
38 |
88 |
||
21 |
Chanika
|
183 |
269 |
33 |
82 |
216 |
351 |
||
22 |
Kanoni
|
63 |
46 |
83 |
44 |
146 |
90 |
||
23 |
Igurwa
|
66 |
108 |
40 |
194 |
106 |
302 |
||
|
jumla |
1755 |
5981 |
882 |
2685 |
2637 |
8666 |
||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.