Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika inaundwa na sehemu tatu (3) ambazo ni:-
MAELEZO YA JUMLA KUHUSU SEKTA YA KILIMO WILAYANI KARAGWE.
Kilimo ni mojawapo ya shughuli za kiuchumi inayochangia wastani asilimia 70 ya pato la Halmashauri. Kaya zinazoshiriki katika shughuli za kilimo ni 61,351 kati ya kaya zote 72,178 za wilaya ya Karagwe. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 108,000 kati ya hekta 4,500,000 ya eneo lote la wilaya. Eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 9,920. Pia idara inashirikiana na wadau mbalimbali waliopo wilayani katika kuendeleza sekta ya kilimo.
Baadhi ya wadau hao wa Kilimo ni K.V.T.C, MAVUNO, CHEMA, WORLD VISION, MATUNDA MEMA, BISHESHE WINW, KARAGWE ESTATE, RADIO KARAGWE, RADIO FADECO, LUKALE WINE, KDCU, KADERES NA OLAM.
LENGO LA IDARA.
Lengo ni kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya biashara na chakula ili kuongeza kipato cha mkulima na kupunguza umasikini.
Idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji inashughulikia masuala ya; Afya za mimea, Ushauri na mafunzo, Uzalishaji wa mazao mbalimbali, Usalama wa mazao ya chakula, lishe na biashara, Biashara ya mazao, Kusimamia vikundi mbalimbali vya uzalishaji na mikopo kupitia SACCOS.
MAJUKUMU YA IDARA
MIKAKATI YA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA
TAARIFA YA MWAKA 2016/2017 IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
Husika na somo tajwa hapo juu.
Ifuatayo ni taarifa ya Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika kwa mwaka 2016/2017.
Mapendekezo/ushauri;
Kilimo cha kahawa
Kahawa ni zao kuu la kibiashara kwa wilaya ya Karagwe na ndilo linaloingizia mapato makubwa halmashauri. Mwaka huu wa fedha halmashauri iliwasaidia wakulima kuwanunulia miche ya kahawa. Lengo kuu ilikuwa ni kufidia mibuni iliyokauka na kuongeza kiasi cha mibuni. Jumla ya miche 115,000 ilinunuliliwa na kugawiwa kwa wakulima 2,300 wa Kahawa katika vijiji 36 mbalimbali hasa vile vilivyokuwa vimeathirika sana na ukame. Shughuli hiyo iligharimu jumla ya Tsh.34,500,000/=
Miche hiyo ilinunuliwa kwa vikundi vya wakulima binafsi vilivyoko hapa wilayani. Hata hivyo vikundi hivyo bado havijalipwa kiasi chochote. Halmashauri inatakiwa ivilipe vikundi hivyo kwa mchanganuo ufuatao.
JUMLA…………………………………………..Tsh.19,579.500/=
Hili ndilo deni ambalo Halmashauri inadaiwa na vikundi vya wakulima wa vitalu vya miche ya Kahawa.
Mafanikio;
Kwa mwaka huu wa fedha tulilenga kukusanya tani 12,000 za Kahawa ya maganda na tukafanikiwa kukusanya tani 9,868 sawa na 82%. Kiasi hicho cha Kahawa kilinunuliwa na makampuni 6 binafisi yaliyoruhusiwa kununua Kahawa wilaya ya Karagwe pamoja na Chama kikuu cha Ushirika KDCU. Makampuni hayo yalinunua kati ya tani1, 200 hadi 1,600 za Kahawa ya maganda
Changamoto katika uzalishaji wa Kahawa
Changamoto Katika Kitengo cha Kilimo na Umwagiliaji
Katika kitengo cha kilimo na Umwagiliaji kuna changa moto mbalimbali zilizojitokeza na kusababisha baadhi ya shughuli kutokutekelezwa kikamilifu. Changamoto hizo ni:
Changamoto katika Kitengo cha Ushirika.
Katika kitengo hiki kuna changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza na bado zinakikabili
Martine, J.L.Nsongoma
Kaimu Mkuu wa idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
Halmashauri ya Wilaya
KARAGWE
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.