Land and Natural Resources
Approximately 68% of residents of Kayanga town and other trading centreslive in unplanned settlements. Land use and environmental managementshould be carried out in accordance with Land, Forest, Fisheries,Beekeeping and Environmental Acts and Policies which are advocatingsustainable use and management of Land and Natural Resources.
Land UseGreater part of the District is cultivated and the remaining are protectedareas (forests, game reserves and ranches). Some patches are leftuncultivated because they are on very steep slopes and some are swampyareas. Livestock keeping is also practiced in wooded and open grasslands.Land is more intensively used in the northern part of the District than in thesouthern part. Deforestation and bush fires are common practices in theDistrict. Tree planting is now becoming common but these efforts arefrustrated by bush fires and livestock grazing by agro pastoralists. Naturalregeneration is the main reforestation mechanism. Due to permanency ofsettlement by the communities, land ownership has been passed from onegeneration to another i.e. land has been transformed to family ownership.Village Governments preserve some land for public uses and provision tolandless people. In most cases women do not own land, due to patri-linealinheritance system but have access to the land of husband.
Functions of the Department:-
Conducting sensitization meetings to urban dwellers.Presenting town planning layouts for approval.Conducting valuations for rating and compensation purposes to allcouncil properties and builings in surveyed plots.To do rating in squatter areas at the urban places.To ensure development of land is in line with land use plans.To provide education on land use/conservation to preserve soil fertility.To sensitize community on proper methods of collection,storage,anddisposal of solid/liquid wastes.To provide and manage contract on environmental sanitation.
TAARIFA YA IDARA YA ARDHI NA MALIASILI KWA
MWAKA WA FEDHA 2016/2017
UTANGULIZI;
Idara ina watumishi 9
Sekta ya ardhi usimamizi imeendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa matumizi bora ya ardhi kwa wananchi kulingana na matumizi ya jamii husika. Sekta imekusanya jumla ya
Tsh 240,863,402.76
Vilevile idara imeahakikisha zoezi la umilikishaji wa viwanja 326 umefanyika na kati ya hivyo jumla ya hati 242 zimekamilika na kuwasilishwa kwa wamiliki wa viwanja husika.
Kitengo kimeendelea kufanya shughuli za kukamilisha zoezi la uandaaji wa hati miliki za kimila kwa wananchi wa kijiji cha nyakayanja na kuendelea kushirikiana na makampuni binafsi katika kufanikisha zoezi la upimaji na uandaaji wa hati miliki za kimila kwa maeneo yaliyopo wilayani.
Zoezi la ukaguzi wa viwanja limefanyika na kutoa notice za maendelezo ya viwanja ambavyo vilikutwa avijaendeleza,ambavyo jumla yake ilikuwa viwanja 293 kwa wilaya nzima,kayanga mjini na kwenye vituo vidogo vya biashara.
Kitengo kimeendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa upimwaji shirikishi kwa wananchi waliopo mamlaka ya mji mdogo kayanga (Katoma-Ruzinga na kitongoji cha Bomani).
Kushiriki katika hatua za awali katika eneo la Kakono ambako inakusudiwa kujengwa bwala la kufufua umeme katika mto kagera eneo la kijiji cha mshabaiguru kata ya Kihanga.
Kazi ya uthamini wa mali za halmashauri umefanyika ikihusisha ardhi,majengo na thamani zilizopo kwenye majengo na ardhi zilizo chini ya usimamizi wa mkurugenzi mtendaji.
Zoezi la upimaji limeendelea ndani ya wilaya kwa kushirikiana na makampuni binafsi(Mataro Land Developers Tnanzania Ltd na Ambon land survey and Geo informatcs co ltd) ambapo kwa mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya viwanja 642 vimepimwa na kati ya hivyo 147 vimekamilika kwa usajili na495 vinasubili kuidhinishwa wizarani ( Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo Ya Makazi).
Upimaji huu umehanyika pia katika vituo vidogo vya biashara Nyaishozi na nyakaiga,ambapo jumla ya viwanja 25 vimepimwa.
Mgogoro wa mipaka kati ya vijiji imefanikiwa kutatuliwa,kati ya kata ya ihembe dhidi ya kata ya Rugu na mgogoro wa mpka katika kata ya nyakasimbi na nyakabanga.
Vilevile kazi ya kuonyesha mipaka katika eneo la hekta 2000 ndani ya eneo la eneo la kulishia mifugo Kitengure,ambalo lilitengwa na serikali kwenda kwenye vijiji vinavyopakana na shamba hilo la mifugo
Mgogoro mwengine ambao ulitafutiwa ufumbuzi wa awali wakati ufumbuzi wa kudumu unatafutwa ni kati ya wakulima na wafugaji katika eneo la MATO lilipo kata ya Nyakahanga na Bugene
Sekta imeendelea kuhamasisha na kuandaa michoro ya mipango miji ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa kayanga na vituo vidogo vya biashara. Kama kuboresha michoro ya awali na kutengeneza mwonekano mpya kulingana na mahitaji na maendelezo ya sasa.
Kwa kushirikiana na sekta nyingine ndani ya idara,imefanya mkutano wa uhamasishaji wa kuandaa mchoro wa mipango mji katika kata ya kanoni,kijiji cha rwambaizi na maeneo yanayopakana ili kupanua mipaka ya kituo kidogo cha biashara.
Sekta imeendelea na zoezi la kudhibiti wanyama hatari na waaribifu ndani ya wilaya
Kutoa elimu kwa wananchi kuusu umuhimu wa uhifadhi na kujikinga na wanyamapori katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya.
Kuendelea kufanya doria na kudhibiti nyara za serikali.
Kutoa elimu juu ya uhifadhi wa misitu na mazao yatokanayo na misitu
Kuendelea kufanya ukaguzi na kusajili wafanyabishara wa mazao ya misitu wilayani.ambapo jumla ya wafanya biashara 25 wamesajliwa kwa mwaka.
Jumla ya Tsh 4,325,490/= zimekusanywa kwa mwaka, ambapo zimetoka na ushuru wa mkaa,mbao na tozo kwa waliokiuka utaratibu.
Jumla ya miti 1, 874,567 imepandwa katika wilaya kwa kushirikiana na taasisi binafsi zinazojihusisha na shughuli za utunzaji wa mazingira, Chema, Agro-forest na watu binafsi.
Ugawaji wa viriba na mbegu(Pine na Gillivelia) kwa baaadhi ya wadau wenye vitalu vya miti na taasisi ambao ni Gereza la kitengule, shule ya sekondari igurwa na shule ya msingi Biyungu.wadau wengine ni kama Chema,Via-agro forest,Himaya na ELECT.
Naomba kuwasilisha
Bernard Essau
Kny; MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA
KARAGWE
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.