DED MSANGA AKAGUA NA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi; Happiness J. Msanga mapema leo September 29, 2025 ameendelea na utaratibu wake wa kawaida wa kuwatembelea wakandarasi kwenye Kandarasi za Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa ikiwa ni sehemu ya kuhimiza ukamilishwaji wa miradi kwa wakati na ubora unaoendana na thamani ya fedha inayotumika.
DED Msanga akiwa ameambatana na Wataalam kutoka Idara ya Ujenzi, Mipango na uratibu, Manunuzi na Afya wametembelea Miradi ya maendeleo inayotekelezwa ikiwemo mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya Bushangaro, Kituo cha Afya Nyakakika, Ujenzi wa miundombinu ya maji, Matundu matatu ya vyoo na kichomea taka katika Zahanati ya Kamagambo, Mradi wa Madarasa matatu ya Shule ya Msingi Nyakashozi na Mradi wa Ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Ahamulama ambayo utekelezaji wake upo katika hatua tofauti kwa lengo la kuwahimiza wakandarasi kuongeza kasi ya kukamilisha miradi kwa wakati ili iweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Bi; Msanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha nyingi Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe zinazolenga kuboresha sekta zote ikiwemo Afya na Elimu.
Aidha, Bi; Msanga ametoa rai kwa wakandarasi kukamilisha miradi kwa wakati ili wananchi waendelee kunufaika na matunda ya Kodi yao na kwamba mkandarasi atakayechelewesha mradi ama Kujenga chini ya kiwango atakumbana na rungu la sheria kwa mujibu wa taratibu.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.