Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha mtoto wa kike habaki nyuma kielimu hasa kwenye kada za sayansi ambazo ushiriki wao ni mdogo kulinganisha na uhitaji wao kwenye taaluma hizo.
Bashungwa ametoa wito huo tarehe 23 Agosti, 2024 wakati wa hotuba yake kwenye Sherehe za Mahafali ya sita (6) ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Mavuno na Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 30 ya Shirika la Mavuno yaliyofanyika viwanja vya shule hiyo, Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.
Bashungwa amesema kuwa Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeadhimia kuwainua Watoto wakike hususani kwenye kada za sayansi ambapo idadi yao ni ndogo mno kwa kuwatengenezea mazingira rafiki ikiwemo kuwajengea shule maalum za wasichana kila mkoa kwa ajili ya masomo ya Sayansi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.
“Nilibahatika kuudhuria kongamano la wahandisi wanawake takwimu zinaonyesha tuna wahandisi wanawake 5,006 tu kati ya 38,233 ambayo ni sawa na 15.07% bado tunahitaji wanawake kuongezeka kwenye taaluma hizi. Niwasihi Wazazi tuendelee kuungana na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwenye jambo hilo habaki nyuma anaendelea kulifanya kwa vitendo” Alisema Bashungwa.
Bashungwa amawasisitiza wazazi kuwekeza kwenye elimu kwa watoto wote ili kuleta matokeo chanya kwa jamii na Taifa.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.