WATHIBITI UBORA WA SHULE, MAAFISA OFISI YA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI KARAGWE DC WANOLEWA MFUMO WA SQAS.
Wathibiti ubora wa shule, Maafisa ofisi ya elimu msingi na sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wamepewa mafunzo ya mfumo wa kidigitali wa kuthibiti ubora wa shule ( School Quality Assurance System- SQAS).
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mkufunzi kutoka Ofisi ya Mthibiti Ubora kwa kushirikiana na Afisa Tehama wa Wilaya yamefanyika mapema leo Julai 10, 2025 katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Elimu Sekondari iliyopo Makao makuu ya Wilaya ya Karagwe.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo ndg. Ndalahwa Masanyiwa ambaye ni Mthibiti ubora wa shule na mkufunzi amesema kuwa matumizi ya mfumo huo yatarahisisha mchakato wa kufanya tathimini za ubora kwa shule, ufuatiliaji maendeleo na kuwezesha utoaji taarifa kwa wadau wa elimu kwa wakati.
Hatahivyo, Takribani Maafisa 13 kutoka ofisi ya wathibiti ubora wa Elimu, Maafisa Elimu Sekondari na Msingi walipata mafunzo hayo.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.