Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imezindua kampeni ya matumizi Safi ya Nishati ya kupikia kwa kugawa bure Mitungi mia tatu ya Gesi kwa wanawake wenye mahitaji maalum, mama lishe, wanawake wajasiriamali, na wanawake wenye ulemavu wa ngozi
Mitungi hiyo imegawiwa na Mbuge wa jimbo la Karagwe na Waziri wa ujenzi Mhe: Innocent Bashungwa ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika shughuli hiyo amesema ugawaji wa majiko ya gesi kwa akinamama wa Wilaya hiyo litakuwa zoezi endelevu ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambavyo huchangia uharibifu wa mazingira na kusababisha Mabadiliko ya tabia nchi..
“Tunaanza na hii mitungi mia tatu kwanza na zoezi hili litakuwa endelevu na kuna mitungi mingine elfu moja itakuja hivi karibu ili kumtua mama kuni kichwani kwa kutumia nishati safi ya kupikia”
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Dr. Amon Mkoga amesema ugawaji wa mitungi hii ya gesi ni kuunga Mkono agenda ya nishati safi ya kupikia ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan na kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni ambayo siyo nishati safi ya kupikia.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.