Na Frank I.Ruhinda
Msanii wa mashairi maarufu hapa nchini Mrisho Mpoto amezuru katika kata za kibondo na Nyaishozi kutoa Elimu juu ya utumiaji wa choo bora.
Bwana Mpoto ameeleza umuhimu wa kutumia choo bora ikiwa ni pamoja na kurinda afya, kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kichocho na kipindupindu.
Aidha kupitia kampeni hiyo imeambatana na michezo tofauti kama Sarakasi, Ngoma pamoja na kuchezesha Nyoka jambo ambalo lilikua linahamasisha wananchi kupitia kampeni hiyo.
Kupitia kampeni hiyo ya “USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO” Wananchi wameonesha kuhamasika kununua sink pamoja na kufuata hatua za unawaji mikono baada ya kutoka chooni kabla ya kula.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.