Na Geofrey A.Kazaula
Wananchi Wilayani Karagwe wameshauriwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya ili kuepuka vifo vya akina mama na watoto.
Hayo yamejiri katika kikao cha Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kilicho kaa kufanya mapitio ya kazi mbalimbali zilizotekelezwa na Idara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali katika kipindi cha Robo ya kwanza 2018/2019.
Sababu mbalimbali zilizotajwa kusababisha vifo vya akina mama na watoto ni pamoja na baadhi ya wananchi kutofuata maelekezo ya wataalam wa Afya ikiwemo kuhudhuria Kliniki na kufuata kanuni za lishe bora ili kupunguza matatizo ya ki afya likiwemo tatizo la udumavu.
Akiafanua zaidi, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Karawge Dr, Christopher Mwasongela amesema kuwa Idara kupitia wataalam wake imekuwa ikitoa maelekezo mara kwa mara na wanaofuata maelekezo ya kitaalam maranyingi wamekuwa hawakumbwi na changamoto za kiafya.
’’ Tumekuwa tukitoa maelekezo mara kwa mara hasa kuhusu afya ya mama na mtoto na maranyingi wanaofuata maelekezo yetu hawakumbwi na changamoto hizo na hujifungua salama watoto wakiwa na afya njema’’ alisema mtaalam huyo.
Katika hatua nyingine wananchi wame aswa kujitokeza mara kwa mara kuchangia damu kwani hakuna njia nyingine ya kupata damu bila watu kuchangia.
Akifafanua juu ya changamoto ya upatikanaji wa damu, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyakahanga Dr Andrew Cesari amesesma kuwa mahitaji ya damu bado ni makubwa licha ya wananchi kusuasua katika uchangiaji wa damu.
’’Tuna hitaji kiasi kikubwa cha damu licha ya wananchi kusuasua katika kuchangia kwani wagonjwa wanao taka kuongezewa damu niwengi hasa pale inapotokea ajali’’alisema mtaalam huyo.
Kwaupande wao, wajumbe wa bodi hiyo wameshauri kuwa elimu iendelee kutolewa kwa umma juu ya uchangiaji wa damu ikiwa ni pamoja na kuelimisha watu mara kwa mara kufuata kanuni za afya bora na maelekezo ya wataalam ili kupunguza changamoto za ki afya katika Wilaya ya Karagwe .
Bodi hiyo pia imepitia mpango na Bajeti ya Idara ya afya kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo kwa mujibu wa Katibu wa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Ndg, Josephat Nkebukwa, bajeti hiyo imelenga kuinua kiwango cha utoaji wa huduma ya afya bora kwa wananchi wa Wilaya ya Karagwe kwa kiwango cha juu.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.