WAKULIMA BUJURUGA WAADHIMISHA SIKUKUU YA MKULIMA KWA KUFANYA MAFUNZO YA VITENDO YA KILIMO BORA CHA MPUNGA.
Leo tarehe 06/06/2025 Wakulima wa Skimu ya Mwisa, Bujuruga Wilayani Karagwe wameadhimisha Sikukuu ya Mkulima kwenye Skimu ya Umwagijiaji (MWISA) kwa kufanya mafunzo ya vitendo ya kilimo bora cha Mpunga.
Mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza uzalishaji wa kilimo cha Mpunga yamefanyika kwenye shamba darasa lililopo kwenye skimu hiyo na kuongozwa na Maafisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwa kushirikiana na Viongozi wa Skimu hiyo.
Akizungumza na Wakulima wakati wa Maadhimisho hayo Kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Kilimo Ndg. Titus Fredinand ambaye pia ni Mpima Afya ya Udongo amesema kuwa ili kupata mazao mengi ni vizuri kupima afya ya udongo na kufuata kanuni za kilimo bora cha Mpunga.
"Kupima Afya ya udongo ni bure. Kuanzia julai tutakuja kuchukua sampuli ili tuwapimie na tutawapa majibu ili kusaidia kuongeza uzalishaji " Alisisitiza Ndg.Titus.
Naye Mhandisi wa Umwagiliaji wa Wilaya ya Karagwe Ndg. Damas Kalisti amewataka Wakulima kufuata maelekezo ya Maafisa Kilimo na Viongozi ili waweze kuona faida kwenye uzalishaji wao.Pia watengeneze vikundi vyenye tija vitakavyowawezesha kupata mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri na Benki za Kilimo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji Mwisa ndg. Crodatus Lazaro amewashukuru Maafisa Kilimo kwa Mafunzo waliyowapatia kuanzia kuandaa shamba mpaka kuvuna na ana amini mafunzo hayo yataongeza thamani ya mazao watakayozalisha hasahasa Mpunga.
Aidha, Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo "Kilimo cha Umwagiliaji, Kilimo cha Uhakika" yaliambatana na kupata chakula cha pamoja.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.