Na , Frank I . Ruhinda.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakasimbi na Shule ya Sekondari Karagwe wametoa elimu kwa wakulima juu ya namna ya kupata mazao ya kutosha kwa kuwataka kufanya utafiti wa kutosha kwenye ardhi na udongo kabla ya kupanda mazao .
Kwa mujibu wa wanafunzi hao, tabia ya udongo hutofautiana na kila udongo unafaa kwa mazao Fulani hivyo wakulima wameshauriwa kutambua aina ya udongo kabla ya kupanda mazao ili waweze kupata mavuno ya kutosha.
Hayo yamejiri katika kilele cha wiki ya elimu iliyo adhimishwa katika shule ya Msingi ya Mtakatifu Peter Clavery inayomilikiwa na Jimbo Katoliki la Kayanga Wilayani Karagwe.
Kwaupande wake Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe ndg, Innocent Nsena amewapongeza wanafunzi hao kwa kutoa elimu ya Kilimo kwa wakulima.
‘’ Nichukue fursa hii kuwapongeza wanafunzi wetu kwa kazi nzuri hasa kuwakumbusha wakulima kulima kwa kuzingatia utafiti ili kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya Uchumi wa Viwanda’’ Alisema kiongozi huyo.
Aidha, aliagiza kuwa kiandaliwe kikao cha pamoja kati ya Shule zilizofanya vizuri ili kupitia mikakati iliyopelekea kufanya vizuri na kuunda mpango Mkakati wa Wilaya ya Karagwe.
Kuhusu makakati wa kutengeneza madawati, Kiongozi huyo aliwataka viongozi, wataalamu na wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada za kutengeneza madawati na kuwezesha wanafunzi kusoma vizuri.
Katika kilele hicho cha Wiki ya Elimu , Shule mbambali zilizofanya vizuri Wilayani Karagwe zilipewa vyeti kama ishara ya kutambua jitihada zilizofanywa na Shule hizo.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.