Na Frank I.Ruhinda
Ukosefu wa elimu juu ya kuhudhuriaVituo cha afya na ukosefu wa damu salama katika hospitari zetu ndicho chazo kikuu cha vifo vya mama wajazito na watoto.
Hayo yameelezwa na katibu wa afya mkoa Bi.Dorosela Njunwa wakati akitoa takwimu katika ukumbi wa vijana Angaza mjini Kayaanga ambapo amesema kuwa mwaka jana vifo vya akina mama na mtoto vilikua 65% na kwa sasa vimefikia 15%
Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt.Michael Mbata amesema ili kuboresha afya za akina mama na mtoto inatakiwa wapewe Elimu juu ya ulaji wa chakula bora ambacho kinaongeza damu na kuepuka dhana potofu ambazo zinasababishwa na waganga wa kienyeji.
Hata hivyo Bw. Mbata amesema kwamba CHF iliyoboreshwa ilianza mwaka 2010 ambapo mtu akilipia alikua na uwezo wa kutibiwa ndani ya mkoa na bakaongeza kuwa vyombo vya habari viandae kipindi maalum ambacho kitakua kinahamasisha wananchi kuchangia katka mifuko ya jamii.
Kadhalika, Abela Bashagi mratibu wa damu salama wilayani Karagwe amesema kuwa hospitali ya wilaya ina uhaba wa unit 277 za damu ambapo watu wengi hupoteza maisha
Mala baada ya kikao hicho kumalizika viongozi wa serikali na wa kijamii waliohudhuria walihamasika kujitolea damu ambapo zilipatikana unit zaidi ya 10.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.