Na Frank I. Ruhinda
Uongozi wilayani Karagwe kwakushirikiana na timu kutoka mkoani, kwa kauli moja wamezindua chanjo ya magonjwa ya watoto ya surua, rubella na polio hasa kwa watoto wa kuanzia miezi tisa hadi kufikia miaka mitano.
Akiongea mbele ya halaiki iliyokuwepo katika kituo cha afya mjini Kayanga Mkuu wa wilaya ya Karagwe kwa niaba ya mkuu wa mkoa Ndg Godfrey Mheruka, amesema chanjo juu ya ugonjwa wa surua imekua ikifanyika kila baada ya miaka mitatu, kuanzia mwaka 1999 hii lea.
Aidha Bw Mheruka amesema kwa zoezi hili kwa magonjwa tajwa hapo juu, wanatarajiwa kutoa huduma kwa walengwa zaidi ya laki nne themanini na sita elfu, na lengo ni kudhibiti milipuko na kutomeza magonjwa hayo.
“Ingawa kiwango cha chanjo kimeendelea kuwa juu, milipuko ya ungonjwa wa surua na rubella imekuwa ikitokea kutokana na ukweli kuwa baadhi ya watoto hawakailishi ratiba ya chanjo” amesema mkuu huyo wa wilaya.
Inasemekana kuwa chanjo ya surua na rubella itakayotolewa inalenga kutokomeza magonjwa, ulemavu na hatimae vifo kwa watoto wetu, jamii inayotuzunguka na hatimae Taifa kwa ujumla.
Magonjwa yanayokingwa kwa chanjo hapa Tanzania kwa sasa ni Kifua kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Polio, Surua, Rubella, Pepopunda, Homa ya ini, Homa ya uti wa mgongo, Kichomi, Kuhara na Saratani ya mlango wa kizazi.
Chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza magonjwa na kupunguza vifo kwa watoto, na hivyo kupunguza gharama kubwa ambazo familia, jamii na Taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Kwa mantiki hiyo, chanjo ni uwekezaji wa kiuchumi katika familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.