Na Innocent E. Mwalo.
Katika kutekeleza maaagizo anuai ya serikali yaliyotolewa hivi karibuni jijini Dodoma na Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Seleman Jafo (Mb) kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya, Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa yote hapa nchini, uongozi wilayani hapa, mnamo tarehe 10/02/2021 uliwaita watendaji wa kata na vijiji kwa ajili ya kuwapa maelekezo juu ya ukusanyaji wa kodi ya majengo, ushuru wa mabango na vitambulisho vya wajasiliamali kama ilivyoagizwa na waziri huyo.
Kikao kazi hicho kilichofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Godfrey Mheluka na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa wilaya yaani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Wallace Mashanda, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Godwin Kitonka na Katibu Tawala wa Wilaya Mh. Innocent Nsena, kwa pamoja walitoa mafunzo na maelekezo kwa watendaji hao wa serikali juu ya zoezi la ukusanyaji wa kodi hizo.
‘’Zoezi la ukusanyaji wa kodi ya majengo linatakiwa kufanywa hapa wilayani kwetu kuanzia tarehe 22/03/2021 mpaka tarehe 5/4/2021 lakini kabla ya hapo linapaswa kuambatana na kampeni maalum ya uandikishaji na uorodheshaji wa nyumba zote za kudumu wilayani hapa’’ aliagiza Mh. Mheluka.
Baada ya maelekezo hayo ya Mh. Mheluka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mh. Godfrey Mheluka alitoa ratiba kwa watendaji hao ambapo pamoja na mambo mengine aliagiza ya kwamba kuanzia tarehe 11/02/2021 hadi tarehe 19/02/2021, watendaji hao wakusanye taarifa kwa kuwaorodhesha wale wote wanaomiliki nyumba za kudumu kwa maeneo yote ya Halmashauri ya wilaya.
Huku akiwakumbusha kutokutumia nguvu katika utekelezaji wa zoezi hasa wakati wa uorodheshwaji wa nyumba hizo, Mh. Kitonkaa alitoa wito kwa wananchi wote wilayani hapa kutoa ushirikiano kwa wananchi wote wenye nyumba za kudumu, kwa wataalam hao ili kukamilishaji zoezi hili lenye nia ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato kwa ili serikali iweze kuboresha ustawi kwa wananchi wote.
Huku akiwatoa wasiwasi, wale wananchi ambao walishalipia kodi za majengo kwa mamlaka ya mapato Tanzania, (TRA), kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Mh. Kitonka aliwaambia wananchi hao kupitia kikao cha viongozi hao ya kwamba hawatalipa mara mbili kodi hizo za majengo bali watapaswa kutunza risiti zao ili zoezi la kulipa litakapoanza wawe na kumbukumbu hizo.
Kupitia kikao hicho Mh. Kitonta aliwajulisha watendaji hao kuwa serikali imekirejesha kwa mara nyingine tena chanzo cha mapato cha ushuru wa mabango kwa mamlaka za seriakli za mitaa kwa ajili ya ukusanyaji na akatoa wito kwa watendaji hao kujipanga kukusanya kwa ajili ya uksanyaji wa ushuru huo wa serikali pamoja na ule wa viatambulisho vya wajasiliamali.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.