Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe wamehamasika zaidi kuendelea kuchanja chanjo ya kujikinga na UVIKO 19. Hii ni kutokana na uhamasishaji unaofanyika kwa ushirika wa watalaam wa afya kutoka Halmashauri (CHMT), Mkoa (RHMT) na wadau wa afya (NGOs). Hamasa hiyo kabambe imeanaza Julai 25, 2022 na kuhitimishwa Agosti 1, 2022 ambapo waliojitokeza kuchanja ni asilimia 107 ya lengo.
Naye kiongozi wa timu ya wataalam kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera, Dkt. Kawia Hassan alisema, “ nakushukuru sana Mkurugenzi Mtendaji kwa ushirikianao wako na kutupa watu sahihi katika kuhamasisha chanjo. Lakini zaidi tunakushukuru kwa kutupa Afisa Habari. Ametusaidia kulitangaza hili zoezi kwe vyombo vya habari na amekuwa akiujuza umma kila tunachofanya kwa kupitia mitandao ya kijamii”. Alisema Dkt. Kawia
Aidha, zoezi la uchanjaji liliendesho katika vituo 20 vya kutolea huduma za afya ijapokuwa huduma inaendelea hata sehemu zinginea ambazo hazikuwa kwenye mpango wa hamasa za uchanjaji.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.