TIMU YA MENEJIMENTI KARAGWE DC YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI HUMO.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bi: Happiness J. Msanga, leo Mei 23, 2025 imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.
Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari Kafunjo iliyopo Kata ya Kamagambo unaotekelezwa na SEQUIP, Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi 80 wenye mahitaji maalum Shule ya Msingi Nyakahanga uliopo Kata ya Bugene unaotekelezwa na Mapato ya ndani, Ujenzi wa Vyumba vya Biashara Stendi ya Bohari Kata ya Bugene unaotekelezwa kwa Mapato ya Ndani, Pamoja na Ujenzi wa Mabweni mawili Shule ya Sekondari Bugene unaotekelezwa na SEQUIP.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.