Selikali ya Tanzania imezuia matumizi ya mifuko ya plastiki (pichani) tangu juni, 2019.Lengo kubwa ni kuokoa mazingira dhidi ya uchafuzi unaotokana na mifuko hio. Kwakuwa maisha yanaendelea selikali ikaleta mifuko mbadala ya kutumia, na mifuko inayokuja imefunga bidhaa (vifungashio) ikaruhusiwa.
Sasa kwa wale wanatumia vifungashio kama vibebeo wanakiuka sheria, wanaotumia mifuko iliyokatazwa kutoka nje ya nchi , wanaoagiza, wanaosambaza na wanaouza wote wanavunja sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 kifungu cha 230 (f) kilichofanyiwa marekebisho tarehe 17/5/2019 na kutangazwa na SELIKALI.
Kwa yoyote atakaye kamatwa anatumia mifuko hio adhabu ni faini kuanzia Tsh 30,000/= hadi Tsh 20,000,000/=, hii ni kulingana na ukubwa wa kosa.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.