Na Innocent Mwalo.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, chini ya Mwenyekiti wake, Mh. Vallence Kasumuni, kwa kauli moja wameazimia suala la usafi wa mazingira kuwa ni moja ya kipaumbele kwa viongozi na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya hii.
Wito huu umetolewa katika kikao kilichofanyika mnamo 07/01/2021, ikiwa ni kikao cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 lakini kikiwa ni kikao cha kwanza wajumbe wa kamati hii ambao ni pamoja na Mh. Wallace Mashanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hii, Mh. Jastin Fidelis, Mh. Evalista Sylivester, Mh. Mugisha Mathias, Mh. Thomas Rwentabaza, Mh. Rwamuhangi Mugasha, Mh. Agnes Melichori, Mh. Jane Bilaro, Mh. Edina Mugasha, Mh. Levina Kibogoyo, Mh. Florian Rwamafa na Mh. Mzakiru tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu Oktoba 2020.
Wajumbe hao kwa kwa kauli moja, wamependekeza kwa uongozi wa wilaya hii na pia wameiagiza menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya kutafakari na kuirejesha siku ya Alhamisi kwa kila wiki kuwa ndio siku ya usafi kama ilivyokuwa hapo awali.
Pamoja na kikao hicho kuazimia juu ya Halmashauri ya wilaya hii kutekeleza mpango wa usafi hasa hasa ule unaohusu mfumo wa kukusanya taka ikiwemo suala la kubaini maeneo maalum ya kutupa taka, wajumbe wa kikao hicho wamesisitiza umuhimu wa wananchi kuhamasishwa juu usafi binafsi wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ambayo huchagizwa sana na uchafu wa mazingira.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.