Na Innocent Mwalo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mnamo 19/01/2021, amefanya ziara ya kikazi wilayani hapa ambapo pamoja na mambo mengine ameweka jiwe la msingi ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa na kusindika chakula cha mifugo (Kahama Fresh) kinachojengwa na mtanzania mzawa, Bw. Jossam Ntangeki wilayani hapa.
Awali katika taarifa yake kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli, Bw. Ntangeki, alimweleza Mhe. Rais ya kwamba mradi huu unatarajia kughalimu kiasi cha shilingi bilioni tisa ikiwemo bilioni 2.7 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo ambapo kwa mra nyingine mmiliki huyo alibainisha ya kwamba baada ya kukamilika kwa mradi huo, kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kusindika lita 10,000 kwa siku na hivyo kuwa na uwezo kuzalisha ajira takribani 400.
Mh. Rais Dkt. Magufuli, katika hotuba yake aliyoitoa kwa wananchi wa Karagwe waliokuwa wamefurika kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika eneo la mradi lililopo kwenye Kata ya Kihanga ili kumsikiliza, alimpongeza Bw. Ntangeki kwa uwekezaji huo na kutoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika ufugaji na uzalishaji wa maziwa kwa kuwa kwa sasa mahitaji ya maziwa kwa watanzania ni makubwa kuliko maziwa yanayozalishwa.
Katika hatua nyingine Mh. Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutangaza haraka zabuni za ujenzi wa kilomita 60 za barabara ya lami ya kuanzia Karagwe kwenda Ngara na ile ya kilomita 50 inayoanzia Kyerwa kuja Karagwe huku pia akimuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera, Mhandisi Andrew Kasamwa kukamilisha ujenzi wa daraja la Kitengule katika eneo la mto Kagera ifikipo Juni 2021.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.