Na Innocent Mwalo.
Katika hali ya kuoneshwa kutokuridhishwa kabisa na namna Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) anavyotekeleza mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Karagwe (KDVTC), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Profesa Joyce Ndalichako (Mb), amemwagiza Bwana Peter Maduki, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Stadi (VETA) kufanya ukaguzi wa kina ili kubaini matumizi ya takribani bilioni nne na milioni mia sita hamsini, (4,650,000,000.00/=) ikiwa ni ghrama zilizopangwa kutumika kujengwa kwa baadhi ya majengo katika chuo hicho.
Huku akionesha kutokufurahishwa kabisa na ujenzi unaoendela katika mradi huu, , kwa nyakati tofauti, katika hotuba yake aliyotoa wakati wa tukio la makabidhiano ya Chuo cha KDVTC kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Chuo (VETA) lililofanyika katika viwanja vya chuo cha KDVTC, Mh. Profesa Ndalichako aliwalaumu TBA kwa kushindwa kutekeleza kwa ufanisi miradi mbalimbali wanayopewa kuifanya na wizara yake.
“Ninyi TBA mna tatizo gani na Wiazara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia? Maana kila mnapopewa mradi wa wizara yangu hakuna mradi unautekeleza kwa ufanisi kama mnavyokumbuka hata mradi wa ujenzi wa majengo ya Mloganzila (sehemu ya chuo kikuu cha Muhimbili) tuligombana sana”, aliuliza Profesa Ndalichako.
Pamoja na kuagiza kufanyika kwa ukaguzi huo, Mh. Profesa Ndalichako aliwalaumu pia TBA kwa kushindwa kukamilisha kwa wakati mradi huo na kuagiza ujenzi huo ukamilika kabla ya ifikiapo mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.
Katika kukubaliana na jambo hilo, Mkuu w Wilaya ya Karagwe, Mh. Godgrey Mheluka alimshukuru Waziri Ndalichako kwa kubaini kasoro na hiyo na kuwaomba TBA kutekelza maagizo ya waziri huyo ili kama kuna fedha itabaki basi itumike kwa matumizi mengine.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.