Na Innocent E. Mwalo.
Mkuu wa Wilaya Karagwe, Mh. Julliet Binyula, amewaomba wananchi wa wilaya ya Karagwe kuwa na subira kutokana na changamoto ya usafiri aina ya dala dala ambayo inawakumba wananchi wa wilaya ya Karagwe kwa sasa kutokana na mabadiliko kadhaa yaliyofanya na dala dala zinazosafirisha abiria kutoka makao makuu ya wilaya mjini Kayanga kwenda kwenye mjini Bukoba kwani Kutokana na muongozo uliotolewa na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu (LATRA), magari yanayosafirisha abiria kutoka mjini Kayanga kwenda mjini Bukoba, safari zake zinapaswa kuanzia kwenye mji wa Omurushaka na sio Kayanga mjini kama iilivyokuwa imezoeleka hapo awali.
Mh. Binyula aliyasema haya kupitia mkutano maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 24/06/2021, katika Ukumbi wa Angaza, alipokuwa akijibu hoja ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Paschal Rwamgata, ambaye alitumia fursa ya muda aliopewa kuzungumza na Baraza hilo keleza juu ya kero katika ya wananchi wa wilaya ya Karagwe hasa wanaotoka katika ukanda wa maeneo ya barabara ya kuelekea Murongo pamoja na wale wanaotoka mjini Kayanga wanaolazimika kwenda Omurushaka na sio kusubiri magari katika maeneo ya Kayanga mjini na Omugakorongo kama ilivyokuwa hapo awali.
‘’Sitaki kuona watu wanateseka, wakati mama Samia [Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania] yupo na mimi msaidizi wake [nikiwa mama] nipo, hivyo kuanzia kesho [tarehe 25/06/2021] nitakutana na Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya na Mkuu wa Polisi wilaya’’, alisitiza Mh. Binyula.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.