Na Innocent E. Mwalo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Godwin Kitonka, ametoa wito kwa wananchi wilayani hapa kuzingatia dhana yakuhusisha makundi yote ya vyakula, kuzingatia ratiba ya kula chakula ikiwa ni pamoja na kula mapema mlo wa jioni kuwa ni silaha muhimu katika maisha.
Kitonka aliyasema haya aliposhiriki kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya mnamo Aprili 26, 2021ambapo pamoja na mambo mengine alitoa ushuhuda juu ya kuibuka kwa wimbi kubwa la magonjwa kwa watu ambao hawazingatii kanuni na ratiba sahihi ya ulaji wa mlo kamili katika ratiba zao za kila siku.
‘’Utashangaa mtu anakula chakula cha usiku majiara ya saa nne usiku tena chakula cha kundi moja au makundi mawili mfano wanga na protini jambo linalounyima mwili makundi mengine muhimu kama vile matunda ambayo kwa kweli kwa kiasi kikubwa yanasaidia sana kulinda mwili’’, alisema Kitonka.
Kupitia hadhara hiyo, Kitonka alishauri juu ya umuhimu wa kula vyakula vya asili vinavyotoka moja kwa moja mashambani badala ya kutegemea vyakula vilivyosindikwa viwandani ambavyo vinakuwa vimeondolewa baadhi ya virutubisho muhimu.
Katika hatua nyingine Kitonka aliwalaumu baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakipuuzia agiza la kuwawezesha watoto wao kukosa kunywa uji shuleni ambapo wazazi hao wamekuwa wakishindwa kuchangia mahindi kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi hao kupata uji na chakula cha mchana mashuleni ambavyo vingesaidia sana katika kupambana na matatizo kama vile utoro na suala la ufaulu hafifu kwa wanafunzi hao.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.