Na Innocent E. Mwalo.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Julieth Binyura, ametoa maagizo mazito ikiwemo katazo la misongamano isiyokuwa lazima wilayani Karagwe kwa lengo la kupambana na kudhibiti wimbi la tatu la maambukizo ya UVIKO-19.
Marufuku hiyo ilitangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Julieth Binyura kupitia mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya, kwa kipindi cha robo ya nne, Aprili - Juni, 2021, uliofanyika katika Ukumbi wa Vijana Rafiki wa Angaza, Julai 27/28, 2021.
Huku akinukuu malekezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, Mh. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), Mh. Binyura, alitoa wito kwa wananchi wilayani hapa kuendelea kuwa wasilivu na kutekeleza maagizo na miongozo ya kujikinga la wimbi hili la tatu la UVIKO-19, kwani ukweli unaonesha kuwa kuna ulegevu wa kukabiliana na janga hili hasa mara baada ya kufanya vizuri na kuvuka salama katika mambapano ya ugonjwa huu yaliyofanywa wakati wa mapambano ya wimbi la kwanza na pili mwaka 2020.
‘’Ndugu wananchi, mtakumbuka kwamba wizara ya Afya imeendelea kusisitiza juu ya kuchukua tahadhali mbalimbali ikiwemo sehemu zote zinazotoa huduma za kijamii zinakuwa na miundiombinu ya huduma ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kama maji hakuna basi kuwe na matumizi ya vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kuzingatia lishe bora pamoja na kufanya mazoezi’’, alielekeza Mh. Binyura.
Mh. Mkuu wa Wilaya aliendelea kutoa maagizo kwa kusema ‘’Kwa hiyo basi kwa kuzingatia kuwa tunakuwa na jitihada za makusudi ya kupambana na maradhi haya naagiza kuanzia leo tarehe 27/07/2021, kuepuka misongamano isiyokuwa na lazima pamoja na kuchukua tahadhali zote kama ilivyoshauriwa na kuelekezwa na Wizara ya Afya’’.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.