MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE AWATAKA WAZAZI WA WANAFUNZI WALIOHITIMU DARASA LA SABA KUWAANDAA WATOTO WAO KWENDA SEKONDARI AU VYUO VYA UFUNDI.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Diwani wa Nyaishozi Mhe:Wallance Mashanda amewataka wazazi wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba kuwaandaa kwenda Shule za Sekondari na vyuo vya ufundi badala ya kuwaacha nyumbani kuolewa au kufanya vibarua.
Mheshimiwa Mashanda ameyasema hayo wakati wa hafla ya mahafali ya darasa la saba ya shule ya Msingi Nyaishozi yaliyofanyika viwanja vya shule hiyo septemba 19,2024 Wilayani Karagwe.Ikumbukwe wanafunzi hao walifanya mitihani yao ya mwisho ya elimu ya Msingi septemba 11 na 12 mwaka huu,wakiwa jumla ya wanafunzi 163 katika shule hiyo.
Mheshimiwa Mashanda ameongeza kuwa Serikali imejipanga vizuri kuwapokea watoto kwenye shule za sekondari na imefanya juhudi mbalimbali kuhakikisha hakuna mtoto atasoma nje kwa kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
“Wazazi naomba tuwajibike kwenye kutengeneza kesho nzuri kwa watoto wetu, Dunia sasa inaenda kasi hasa kwenye matumizi ya sayansi na teknolojia unapoacha mtoto wako nyumbani au kumshawishi afanye vibaya shuleni ukumbuke kuna kesho utazeeka au hutakuepo kabisa utamuacha mtoto kwenye mateso.Watoto hawa bado ni wadogo wanahitaji malezi na ikiwezekana tuchochee vipaji vyao ili waweze kuenda na kasi ya dunia” alisema Mashanda
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ndugu Hosea Mbulamagyo,amewataka wanafunzi kuendeleza tabia njema walizojifunza wakiwa shuleni na waendelee kuishi kwa kufuata maadili mema kwani jamii inawatazama na amewasisitiza kuepukana na tamaa za dunia,nendeni hvyo hvyo na mjiande kwenda sekondari na endapo watapangiwa shule za Sekondari wasiache kwenda na amewasihi wazazi kuacha kuficha watoto .
Hata hivyo,Mhe: Wallece Mashanda alitumia jukwaa hilo kuwakumbusha wananchi kuhusu ujio wa Mwenge Uhuru Wilayani Karagwe utakaofanyika Septemba 24,2024 na Uchaguzi wa Serikali zaMitaaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.