Na Innocent E. Mwalo.
Ikiwa ni Mpango wa Tatu, Sehemu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini, (TASAF), uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, Julai 17,2020, utekelezwaji wa mradi huu wilayani Karagwe unatajwa kuwa umefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo hadi sasa umefikia dirisha la tatu tangu shughuli za mradi huu zilipoanza wakati huo.
Takwimu zilizotolewa mnamo tarehe 19/02/202 na Mratibu wa Mradi huu wilayani hapa, bwana Edius Rwangonga, zilionesha kuwa jumla ya shillingi 444,864,000 zimepokelewa na zinatajiwa kuhawilishwa kwa wanufaika wapatao 8,195 kwa dirisha la tatu linalofanyika mwezi Februari 2021 ikiwa orodha ya walengwa waliohakikiwa katika Mpango wa Tasafi Awamu ya Tatu, sehemu ya pili ya kuanza kwa zoezi la kuhawilishwa kwa fedha hizo.
Kwa upande mwingine bwana Rwangoga alibainisha kwamba mradi huu wa TASAF Awamu ya Tatu, Sehemu ya Pili utakuwa na tofauti na kidogo na ile ilitekelezwa katika Awamu za Kwanza na za Pili kutokana na ukweli kwamba utekelezaji wa Awamu ya Tatu sehemu ya Pili umejikita na kusisitizwa kwa walengwa kuwekeza katika miradi midogomigo na ya kati ili iweze kuwasaidia kujipatia mahitaji yao muhimu.
‘Katika TASAF Awamu ya Tatu, sehemu ya pili ruzuku zitakazotolewa zitajikita zaidi katika miradi ya maedeleo katika sekta za elimu, afya na hasa upatikanaji wa Bima ya Afya ya CHFili kuwa na uhakika wa huduma ya afya na miundombinu’’, alisisitiza bwana Rwangoga.
Nao wanufaika wa mpango huu wa TASAF awamu ya Tatu, Sehemu ya Pili, kwa upnade mmoja walielezea kufurahishwa kwao na ruzuku hiyo inayotolewa na serikali ambapo waleelezea jinsi watakavyonuifa na ruzuku hiyo.
Mlengwa mmoja aliyejitambulisha kwa majina Levina Murashani kutoka Kayanga alisema yeye kama mama ambaye ana watoto watatu, ruzuku hiyo imemsaidia katika matumizi ya watoto haswa mahitaji ya shule ambapo alitoa ushuhuda kuwa kupitia ruzuku ya fedha hiyo ya TASAF imeweza kumsaidia kumudu kusomesha mtoto wake hadi kufikia elimu ya chuo Kikuu.
Mlengwa mwingine, bwana Mpembelege Zemambo wa kijiji cha Bugene alikiri kunufaika na mradi huu ambapo alibainisha kuwa mbali na kupata mahitaji ya watoto ameweza kuanzisha mradi wa ufugaji kuku ambao humsaidia kujipatia mahitaji mengine mengine ya kifamilia.
Kwa upande wake Bi. Amida Mjagala ambaye ni Afisa Mhawilishaji wa fedha hizo za ruzuku za TASAF mbali na kukiri kuwepo kwa changamoto kwa kiasi fulani kwa baadhi ya walengwa kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, alieleza kwamba kwa kiasi kikubwa walengwa wengi wamekuwa wakitumia ruzuku hiyo vizuri huku akibanisha ya mafano wa kuwa na walengwa katika eneo lake walioweza kujenga nyumba za mabati na hivyo kuondokana na adha ya kunyeshewa na mvua kwani hapo awalin walikuwa wanaishi kwenye nyumba zilizoezekwa na nyasi.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.