Na Innocent E. Mwalo.
Ikiwa ni kutaka kujionea mwenyewe bila kutegemea kuletewa taarifa mezani, Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mh. Meja Jenerali Charles Mbuge, Julai 9, 2021, akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Mh. Profesa Faustine Kamuzora pamoja na wajumbe wote wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa walifika wilayani Karagwe na kutembelea eneo tarajali kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Kagera katika kijiji cha Rwambaizi.
Katika hali ya kuonesha kufurahishwa na mandhari ya eneo hilo pamoja na ukubwa wa eneo la ekari 57 zilizotengwa wa wananchi wa kijiji cha Rwambaizi kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mkuu, Mh. Meja Jenerali Mbuge alionesha kufurahishwa na mapokeo ya wananchi wa kijiji hicho juu ya ujenzi wa maradi huo.
Wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kumsikiliza Mh. mkuu wa mkoa na ujumbe wake, katika eneo hilo la maradi tarajiwa, chini ya uongozi wa mwenyekiti wa kijiji hicho cha Rwambaizi ndugu George Francis na diwani wa kata ya Kanoni Mh. Frolian Rwamafa, kwa kauli moja waliridhia kujengwa kwa shule hiyo huku wakimhakikishia, Mh. Meja Jenerali Mbuge kuwa wapo tayari kushirikiana na serikali katika ujenzi wa mradi huo na pia walimhakikishia mkuu wa mkoa ya kwamba eneo lote walilolitoa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo halina mgogoro wowote.
Katika hatua nyingine Mh. Meja Jenerali Mbuge na msafara wake walitembelea miradi mingine miwili inayotekelezwa hapa wilayani ya Karagwe ambapo miradi hiyo ilikuwa ni ujenzi wa wodi tatu katika hospitali ya wilaya (eneo la Nyakanongo) na ujenzi wa baadhi ya majengo katika chuo cha Ufundi Stadi cha Karagwe (KDVTC)
Pamoja na kuonesha kuridhishwa na mendeleo ya miradi hiyo miwili, Mh. Meja Jenerali Mbuge kwa nayakati tofauti alitoa maelekezo na maagizo kadhaa ambapo katika chuo cha KDVTC alimwagiza msimamizi wa maradi huo, wakala wa majengo (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Salum Chanzi kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kabla au ifikikapomwezi Septemba mwaka huu huku akirudi kuukagua mradi miezi miwili baada ya kukamilika kwake.
Aidha katika mradi wa ujenzi wa wodi tatu katika hospitali ya wilaya, Mh. Meja Jenerali Mbuge alitoa maagizo kwa menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Karagwe ambao ndio wasimamizi wa ujenzi wa mradi huo kuhakikisha mandhari ya eneo hilo yanafanyiwa usafi pamoja na kupandwa maua ili ubora wa majengo hayo ufanane na mazingiora yanayolizunguka eneo hilo.
‘’Nimeona jitihada zinazoendele katika mradi huu pamoja na mambo mengine mliyonieleza kupitia taarifa yebnu ya ujenzi napenda kuwaagiza kuwa ujenzi wa neo hiklo uwe umekamilika kblaau ifikapo mwezi wa nanAgosti mwaka huu ili dhamira ya serikali kuwapa wananchui hyuduyuma hii ya afya uwezekutimi’’, aliesema Mh. Meja Jenerali Mbuge.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.