Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Bw. Michael Nzyungu amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa majengo ya hospitali ya wilaya, kukagua mapato ya mnada wa mifugo na mageti ya mapato.
Ziara hiyo ameifanya Juni 17, 2022 akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya mapato (task force). Mnadani alibaini wafanyabiashara zinginezo tofauti na mifugo hawalipii ushuru wa gulio na wala hawana vitambulisho vya ujasiriamali.
“Haiwezekani wafanya biashara wa gulioni kufanya biashara bila kulipia ushuru wa Halmashauri. Huko nilipokuwa walikuwa wanalipia shilingi 2,000/= kwa kila mfanya biashara kama ushuru wa gulio”. Alisema Bw. Nzyungu.
Aidha, amewaagiza wafanyakazi wote kwenye vizuizi vya mapato kuhakikisha wanakuwa waaminifu na kutokuruhusu kahawa kutoroshwa pasipo kulipiwa na kwenda wilaya jirani.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.