Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Bi. Happiness J. Msanga mapema leo Agosti 29, 2024 amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya karagwe lengo likiwa ni kupokea changamoto mbalimbali kutoka kwa watumishi hao na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha na kuleta ufanisi katika utendaji kazi.
Akiongoza kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Angaza Bi. Happiness Msanga amewasisitiza wakuu wa Idara na vitengo kutumia OC zao kununua vitendea kazi vya ofisi na kuweka mazingira rafiki kwa watumishi wao wa chini na kuishi kwa kushirikiana na kwa upendo ili waweze kutoe huduma bora kwa Wananchi.
Pia amewasisitiza Watumishi kuwa na nidhamu, maadili na utiifu wakati wa kazi na kuwahi kazini kwa mujibu wa sheria, kuzingatia mavazi yenye maadili kama mtumishi wa umma na namna nzuri ya kuwasiliana hasa kwa kutumia maandishi na kufuata cheni ya mawasiliano
“Tufanye kazi sisi ni watumishi wa umma tuache majungu tupendane na hasa huko kwenye idara zenu na vitengo tuonyeshane upendo na tufanye kazi kwa moyo mmoja”
Vile vile Mkurugenzi Bi. Happiness Msanga amewasisitiza watumishi juu ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA na masuala ya manunuzi yote yafanyike kwenye mfumo sababu teknolojia inabadilika kwa hiyo watumishi tutii sheria na utaratibu uliowekwa na pia kutumia vizuri mfumo wa pepmis ili ukusaidie kupata promosheni
Aidha Bi. Msanga ameongeza kwa kuwaomba Watumishi wafanye kazi kama timu na kuahidi Kuunda kikosi kazi cha ukusanyaji wa mapato na ili tuweze kuishi kwa amani na furaha ni lazima tukusanye kwa wingi kwani mapato ndiyo njia ya kuondoa kero ndogo ndogo hasa hili suala la madeni ya watumishi
Kwa upande wa watumishi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali ikiwemo ya madeni yao, uhaba wa vitendea kazi, upandaji wa madaraja, kubadilishiwa muundo na siku za mapumziko na kupatiwa majibu na ufafanunuzi wa maswali yao
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.