Na Innocent E. Mwalo.
Katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na mijini yenye mawasiliano hafifu kama ilivyo kauli mbiu yao isemayo ‘’Mawasiliano kwa Wote’’, Mfuko wa Mawasiano kwa Wote, UCSFA, umepanga katika kipindi cha mwaka 2021 kujenga minara saba ya simu katika eneo la hifadhi ya Kimisi wilayani hapa ili kutengeneza mfumo wa upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano.
Hayo yalibainishwa na Mhandisi Francis Mihayo, mjumbe wa Bodi ya UCSFA, katika kikao kilichofanyika kati ya taasisi hiyo na uongozi wa wilaya ya Karagwe mnamo 6/2/2021 katika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya.
Katika kikao hicho, kilichowashirikisha pia wajumbe wa Bodi ya Mfuko huo, wakiwemo ndugu Francis Chachah, Gerald Matee, Lawrence Mworia na Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Bi. Justina Mashiba pamoja na mambo mengine waliweza kuelezea juu ya utekelezwaji wa miradi anuai ya mawasiliano katika kata 17 za wilaya hii ikiwemo kata ya Igurwa, Kanoni, Ihembe, Rugu na Bweranyanga.
Aidha katika kujibu hoja ya Katibu Tawala wa Wilaya, Mh. Innocent Nsena pamoja na washiriki wengine kutoka wilayani hapa ambao walielezea jinsi mawasiliano ya simu na redio yalivyo na changamoto katika wilaya hii, Mhandisi Mihayo pamoja na mambo mengine alibainisha kwamba tayari taasisi yake imekwisha sainiana mkataba na Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC, ili kuboresha usikivu wa redio hiyo hasa katika maeneo yote pembezoni yenye changamoto kubwa ya kutokupata mawasiliano au kupata mawasiano ya simu na redio kutoka nchi jirani ambazo maeneo hayo yanapakana nazo.
‘’Pamoja na kwamba taasisi yetu ni tasisi ya serikali lakini tunalo jukumu la kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu’’, alisikika Mhandisi Mihayo akijibu swali la mshiriki mmojawapo wa kikao.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.