Na Innocent Mwalo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Mh. Wallace Mashanda, mnamo tarehe 09/01/2021, ametoa maombi maalum matatu kwa Waziri wa Ellimu, Sayansi na Teknolojia, Mh. Joyce Ndalichako (Mb) ili kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya elimu wilayani Karagwe.
Katika hotuba yake aliyotoa wakati wa tukio la makabidhiano ya Chuo cha KDVTC kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Chuo (VETA) yaliyofanyikia katika viwanja vya chuo cha KDVTC, Mh. Mashanda alizitaja changamoto tatu zinazoitafuna sekta ya elimu wilayani hapa ikiwemo upungufu wa walimu takribani 1, 000 kwa shule za msingi na upungufu mwigine ni ule wa walimu wa masomo ya sayansi kwa shule za sekondari.
“Mh. Waziri pia tunahitaji msaada wa serikali kuu katika kukamilisha ujenzi wa maboma 35 ya maabara ambapo ujenzi wake umefika takribani asilimia 70 ikiwa ni nguvu za wananchi na tatizo jingine la tatu ni kukosekana kabisa kwa shule za sekondari za kidato cha tano wilayani hapa”, alisisitiza Mh. Mashanda.
Aidha katika kuelezea utatuzi wa changamoto ya kukosekana kwa shule za serikali sekondari za kidato cha tano na cha sita wilayani hapa, Mh. Mashanda alitoa maombi kwa Mh. Profesa Ndalichako kufanyiwa kazi kwa mapendekezo ya uanzishwaji wa shule za sekondari za Kituntu, Nyakasimbi na Nyabiyonza ili ziweze kuwa za kidato cha tano na cha sita.
Katika hatuna nyingine Profesa Ndalichako alikubaliana na maombi yaliyotolewa na Mh. Mashanda na kusisitiza kwamba tayari kilio hicho kilikuwa kimemfikia kupitia Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mh. Innocent Lugha Bashungwa ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na hivyo kuwaahidi wananchi wa Karagwe kuzifanyia kazi changamoto hizo kadri itakavyowezekana.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.