Na Frank I. Ruhinda
Makampuni ya ulinzi Wilayani Karagwe yameagiza kuajiri wahitimu wa mafunzo ya mgambo kwani ndio wenye sifa, wala sio kuajiri ndugu zao wasio kuwa na sifa wala mafunzo yoyote ya kijeshi.
Maagizo hayo yametolewa mwishoni mwa wiki wakati wa kuapisha wanamgambo hao katika uwanja wa changarawe mjini Kayanga Karagwe.
Akitoa maagizo hayo Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka amesema makampuni yote ya ulinzi wilayani Karagwe, yanapaswa kuajiri hawa vijana waliojitolea kwa moyo kufunzwa mafunzo ya mgambo na sio kupendelea ndugu zao tena kutoka nje ya wilaya yetu saa nyingine ata hao ndugu zao hawana mafunzo yoyote ya kijeshi na watu wenye sifa wanaachwa hapa wilayani kwetu.
“Tuwe wazalendo jamani ivi unajisikiaje unapomuita ndugu yako kutoka huko huku ukijua kuawa mtu huyo hana sifa ata chembe na mwenye sifa ni jirani yako hapa unapoishi” alisema mgeni rasimi.
Katika risara ya wahitimu wa mafunzo hayo ya mgambo iliyosomwa na Briliant Meena ilisema miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na kukosa kazi, na wale waliopata kazi kucheleweshewa mishahara au kunyimwa kabisa hadi kukimbilia kwenye vyombo vya sheria.
Mafunzo hayo yametolewa kwa kipindi cha miezi sita, huku wanamgambo walioanza mafunzo walikuwa jumla 335 na waliohitimu walikuwa jumla 244.
Aidha mshauri wa mgambo wa wilaya aliwaasa wahitimu hao wa jeshi laakiba kuwa wasiende kuleta ubabe wa mafunzo ndani ya jamii inayowazunguka badala yake wanapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kusaidiana na jeshi la polisi kulinda amani.
Baada ya Mkuu wa wilaya kufunga mafunzo hayo alitoa zawadi kwa badhi ya wahitimu hao waliofanya vizuri zaidi katika badhi ya vitu kwa mfano kama kulenga shabaha, kuwa na nidhamu na vitu vingine.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.