MADIWANI WAPONGEZA WATUMISHI UKUSANYAJI MAPATO 2022
Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji na watumishi kwa kukusanya asilimia 109 ya mapato ya ndani. Pongezi hizo zimetolewa Julai 28, 2022 kwenye kikao cha Baraza la robo ya nne kwa mwaka 2021/2022 katika ukumbi wa Angaza.
Akiwa anafungua kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mhe. Wallace Mashanda alisema, “ kwa mara ya kwanza Halmashauri kukusanya zaidi ya asilimia 100. Miaka ya nyuma tulikuwa tunaishia asilimia 78 lakini kwa Mkurugenzi wa sasa tunaona tunasonga mbele. Tunampongeza kwa kweli yeye pamoja na watumishi wanaomsaidia kukusanya mapato”.
Aidha, baraza hilo la madiwani liliongeza kuwa kazi ya mapato ni ngumu lakini tuendelee kusonga mbele kwani ukusanyaji wa mapato ni vita na njia pekee ya kuishinda ni kufuata sheria, kanuni na taratibu.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.