MABONDIA 4 KUIWAKILISHA KARAGWE DC KWENYE MCHUJO WA KUTAFUTA TIMU YA MASUMBWI YA MKOA WA KAGERA.
Mabondia wa 4 ambao ni Patson Pancras, Ibrahim Hassan, Joel Joseph na Hassan Keffa wanatarajia kuiwakilisha Wilaya ya Karagwe kwenye mashindano ya mchujo wa kutafuta timu ya Masumbwi ya Mkoa wa Kagera yatakayofanyika kesho Tarehe 01/03/2025 katika Ukumbi wa Linus, Mjini Bukoba.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wakati wa kuaga Mabondia hao, Afisa Michezo George Sebastian amewatakia ushindi mabondia hao na kutoa wito kwa vijana wengine hasa wasio na ajira kujiunga na mafunzo ya michezo ya Masumbwi kwani kwasasa sio mchezo tu bali ni fursa ya ajira.
Aidha, Mwalimu wa Mchezo huo Kocha Sixbert Magambo amesema kuwa hii ni mara yao kwanza kushiriki mchujo huu na wanatarajia kuitumia fursa hiyo vizuri kuhakikisha wanafika ngazi ya Mkoa na Taifa kwenye mchezo huo.
"Maandalizi ya mchezo wa ngumi ni mazoezi, Sisi tumejiandaa na tunategemea kuiwakilisha vizuri Wilaya yetu ya Karagwe ili tupate nafasi ya kuwa kwenye timu ya Mkoa na hata Taifa" Alisema Kocha Sixbert.
Kwa upande wake, Bondia Joel Joseph ambaye alizungumza kwa niaba ya mabondia watakao iwakilisha Wilaya ya Karagwe amesema kuwa, kikosi kimejiandaa kwa muda mrefu na kiko vizuri na kipo tayari kuitetea Wilaya kwenye mashindano hayo.
Hatahivyo, Mashindano hayo yatahusisha Wilaya zote 8 za Mkoa wa Kagera ikiwemo Karagwe, Ngara, Biharamulo, Missenyi, Muleba, Bukoba Manispaa, Bukoba Vijijini na Kyerwa.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.