Na Innocent E. Mwalo.
Maandalizi ya Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 202 ambao utapokelewa katika wilaya ya Karagwe Oktoba 3, 2021, ukitokea katika wilaya ya Ngara, yamepamba moto ambapo Kamati ya Mwenge wilaya chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Julieth Binyura, tarehe 30/07/2021, wametembelea miradi mbalimbali ambayo mbio za mwenge wa uhuru zitaweka jiwe la msingi, kuzindua pamoja kukagua miradi hiyo.
Kazi hiyo ya kutembelea miradi hiyo ilifanywa katika meneo ya Kata za Nyakasimbi, Rugu, Nyaishozi, Bugene na Kayanga ambapo katika maeneo hayo miradi inayohusu sekta za afya, kilimo, misitu, mapambano dhidi ya UKIMWI na lishe ambapo Mwenge wa Uhuru 2021 utapita kukagua, kuzindua na kuweka jiwe la msingi.
Aidha kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2021, isemayo’’TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu Itumike kwa usahihina Uwajikaji’’, mwenge wa uhuru utatemebelea miaradi mbalimbali kama vile usajili wa wakulima kupitia mfumo wa ki-elektroniki.
Miradi mingine ni pamoja na klabu ya wapinga rushwa, miradi ya sekta ya maji, miradi ya ujenzi wa barabara za vijijini na mjini pamoja na miradi iliyotokana na ukopeshaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Katika majumuisho ya ziara hiyo, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya, Mh. Binyura alisisitiza kwa kusema, ‘’ Tumetemebelea miradi ila bado tuna changamoto ya kuibua/ kutafuta miradi bora zaidi, kwa hiyo nawaagiza wataalam wa Halmashauri na Idara nyingine za serikali kuendelea kubuni zaidi miradi’’.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.