MAOFISA KILIMO 9 WAKABIDHIWA PIKIPIKI ILI KURAHISHA NA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI SEKTA YA KILIMO.
Maofisa Kilimo 9 za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wamekabidhiwa pikipiki ambazo zimetoka Wizara ya Kilimo kwa ikiwa ni muendelezo wa kuwawezesha na kuongezea ufanisi katika utendaji kazi Maafisa Ugani Nchini.Makabidhiano hayo yamefanyika makao makuu ya Halmashauri yaliyopo kata ya Kayanga.
Akizungumza katika halfa hiyo ya makabidhiano MKurugenzi Mtendaji Bi.Happiness Msanga ameishukuru Serekali kupitia Wizara Ya Kilimo kwa kuendelea kuwakumbuka watumishi wa Wilaya Ya Karagwe hususani maafisa ugani ngazi ya kata ambao shughuli zao kwa kiasi kikubwa zinategemea usafiri kutokana na ukubwa wa maeneo na umbali ili kuwafikia wananchi kwa wakati.
“Nichukue nafasi hii kuwasisitiza maofisa wote ambao mmekabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kufanikisha kazi zenu mzitunze na kuzitumia kama ilivyokusudiwa,sitegemei kuona mnazitumia kama boda boda au kwa matumizi yenu binafsi zaidi badala ya kuwatumikia wananchi ambao ndio walengwa.Pia niwakumbushe kuhakikisha mnaleseni halali na mmeudhuria mafunzo kwa wale ambao hamjui kuzitumia ili pikipiki hizi zisiwe sababu ya ajali,nategemea matumizi salama na mtazingatia Sheria za Usalama Barabarabani ili kuepukana na ajali zisizo za lazima” Alisisitiza Bi.Msanga.
Naye,Afisa Kilimo kata ya Kayanga ndugu Fatuma Hashimu akiongea kwa niaba ya maafisa kilimo waliokabidhiwa pikipiki hizo,ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kuwapatia pikipiki ambazo zitawasaidia kuwafikia wakulima kwa haraka zaidi na kutatua changamoto zao kwa wakati ukilinganisha na awali ambapo hawakuwa na chombo cha usafiri.
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ina maafisa ugani 33 ambapo tayari maafisa 24 walishakabidhiwa pikipiki,na 9 ambao ni waajiriwa wa hivi karibuni ndio waliokabidhiwa leo ,hii ikiwa ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi kwa watumishi wa umma katika kuongeza ufanisi na weledi katika kutimiza majukumu yao ya kila siku.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.