MAADHIMISHA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI YATAMATIKA WILAYANI KARAGWE.
Kilele cha Maadhimisho ya Elimu ya Watu Wazima kwa Mkoa wa Kagera kimefanyika katika Halmashauri ya Wilaya Karagwe kwenye viwanja vya stendi ya mabasi Kayanga tarehe 04 oktoba 2024.
Maadhimisho haya yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujumuishi katika elimu bila ukomo kwa ujuzi, kwa ustawi, amani na maendeleo” yalifunguliwa rasmi Oktoba 02, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na kuhitimishwa 0ktoba 04, 2024 ambapo mgeni rasmi alikua Afisa Taaluma wa Mkoa ndugu Michael Lugola ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bi.Fatma Hajat Mwassa
Hafla hii ilihusisha Wilaya zote saba za Mkoa wa Kagera ambazo ni Biharamulo, Bukoba mc, Bukoba, Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Ngara na Kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya hizo akiwemo Mkufunzi mkazi wa Mkoa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karagwe, Wakuu wa idara za elimu ya msingi na sekondari, na maafisa elimu ya watu wazima kutoka Mkoa wa Kagera Pia, walimu wa shule za msingi na sekondari,Vyuo vya ufundi, wajasirialiamali,wawakilishi kutoka taasisi za fedha na benki, Wananchi, pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na elimu ya watu wazima.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, ndugu Michael Lugola alianza kwa kuelezea lengo la elimu ya watu wazima ambapo alisema ilenga kuto aelimu kwa watoto na watu wazima waliokosa nafasi kwenye mfumo rasmi wa elimu ambapo hujifunza kusoma,kuandika,ufundI stadi na ujuzi utakawawezesha kumudu maisha yao.Maadhimisho hayo ni utekelezaji wa sera ya utekelezaji wa sekta ya elimu unao akisi malengo ya dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025 inayolenga watu wote kujua kusoma na kuandika
“Wito kwa wananchi wa kagera ni kutumia fursa inayotolewa na Serikali kuhakikisha wote tunaelimika kupitia hii programu ya Elimu ya watu wazima na niwasihi wazazi na walezi wasitumie fursa hii kama sababu ya kutosimamia matakwa ya sera ya Elimu kwa watoto wenye umri wa kuwa kwenye mfumo rasmi kama ilivyoanishwa kwenye sera ya elimu ya mwaka 2004 na marekebisho yake ya mwaka 2014 na kuhakikisha uandikishwaj wa lazima kwa watoto unafanyika ambapo umeanza septemba na utamalizika disemba” alinukuu ndugu Lugola.
Aidha, Ndg: Michael Lugola alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho na kushuhudia namna vituo vya elimu ya watu wazima vinavyofanya kazi na elimu za ufundi zinatolewa pamoja na kuona baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na vituo hivyo. Mabanda yaliyokuwa eneo la maadhimisho ni banda la chuo cha Veta Karagwe (KDVTC), Fuxang heath care, Banda la CRDB, YES group, Wapambajina Arumas Open School ambapo aliwapongeza kwa juhudi zao na kuwahimiza kuendelea kuongeza bidii katika kazi zao ili kuboresha ubora wa bidhaa zao, kuwa na ushindani katika soko, na kudumisha dhamira ya kujifunza kila siku, kwani hii ndiyo nguzo ya elimu ya watu wazima.
Hatahivyo, Kupitia hotuba hiyo alikumbushia ushiriki wa Uchaguzi wa Serikali za MItaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 na kusisitiza watu wakajiandikishe kwenye daftari la makazi ambalo ndilo litakalowawezesha kushiriki uchaguzi huo utakaoanza oktoba 11 hadi 20, 2024.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.