KIKAO CHA TATHIMINI YA SHUGHULI ZA LISHE KWA ROBO YA PILI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Ndg. Jackson Mwakisu leo mapema Tarehe 23/1/2025 ameongoza kikao cha tathimini ya shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya pili kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba,2024.
Aidha, Ndg; Mwakisu amewataka wajumbe hao kuendelea kutoa elimu na kila mmoja atimize wajibu wake ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Pia amevishukru vyombo vya habari vya kijamii kwa kuendelea kutoa elimu sahii ya lishe na mambo mengine kwa uharaka akiwaomba watumishi wa ngazi zote kuwaeleza wananchi kufuatilia elimu hizo. Hata hivyo Mwakisu amewataka wanaume kuondoa mfumo dume na kushiriki huduma za malezi kwa watoto wao na kuwasisitiza maafisa ugani kuendelee kuwahimiza wananchi kulima vyakula vya kutosha na kuchangia chakula mashuleni ili Watoto wetu waendelee kupata chakula Shuleni.
“Kwahiyo suala la lishe tunavyokaa hapa sisi, tunajadiliana mustakabali wa maendeleo ya Halmashauri yetu. Watoto wetu wa baadae waje kuwa na akili, wafanye mambo makubwa kwa ajili ya Nchi yetu”
Akisoma taarifa ya Lishe kwa robo ya pili Oktoba Desemba Afisa Lishe wa Wilaya ya Karagwe Bi. Asnath Thobias ameeleza shughuli zilizofanywa na idara hiyo kwa robo hii ya pili ikiwa ni ununuzi na Ufungaji wa Mashine 4 za kuongeza virutubishi Kwenye unga wa mahindi katika shule tatu za sekondari (Sekondari ya Ihembe, Kawela, Nyabiyonza na mdau mmoja Kata ya Nyakahanga) pia aliwasisitiza Wanaume kushiriki katika matukio mbalimbali ya Lishe katika jamii Kwani wanaume ndiyo wanao toa maamuzi ndani ya familia.
Aidha, Mganga mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dr. Agness Mwaifuge ameishauri kamati ya lishe ya Wilaya kuendelea kutoa elimu kwenye jamii juu ya vyakula sahii ili kuondokana na magonjwa ya utapiamlo na udumavu na kama wajumbe wa kamati ya lishe wasione aibu katika kuwaelimisha wananchi ili kuwa na watoto wasio na udumavu, Wito huo ameutoa kwenye kikao cha kawaida cha robo ya pili Oktoba- Novemba 2024 kilichoketi katika ukumbi wa angaza mjini Kayanga.
Kupitia kikao hicho wajumbe wa kamati ya lishe Wilaya ya Karagwe wameeleza namna walivyotekeleza shughuli za lishe kwa kipindi hicho kupitia sekta na taasisi zao ambapo Afisa Maendeleo Ya Jamii Bi; Henrieta Wiliam alieleza kwenye kikao hicho wameendelea kuhamasisha jamii kujihusisha na kilimo ili kupata chakula Cha kutosha katika kaya na kuendelea kupata mlo Kamili na Wananchi kujishughurisha katika masuala ya kiuchumi Kwa kusajili vikundi kwaajili ya kupata mikopo ili kuimarisha uchumi ndani ya familia.
Aidha, Kaimu Afisa kilimo wa Wilaya ya Karagwe Ndg; Yustadi Dominic akiwasilisha taarifa ya idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wameendelea kuwaelimisha wananchi Kutunza mashamba, kutengeneza bustani za mbogamboga majumban kwao ili kuongeza uzalishaji wa mbogamboga, kilimo Cha viazi Lishe, ulaji wa Samaki, na ufugaji wa wanyama hasa ngombe na mbuzi kwaajili ya unywaji wa maziwa jumla ya mabwawa 65 ya ufugaji wa Samaki ambapo Kwa kipindi Cha Oktoba Desemba kilo 265 za samaki zimevunwa ili kuongeza Lishe Bora katika jamii.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.