Na Innocent E. Mwalo.
Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC), chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Mh. Godfrey Mheluka, mnamo tarehe 17/02/2021 imejadili na kutoa ushauri na mapendekezo kadhaa juu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ili Halmashauri iweze kukusanya kiasi cha takribani bilioni 2, 671,904,000.00 ambazo ni mapato ya ndani na hivyo kufikia lengo la kuwa na bajeti ya mapato na matumizi ya takribani bilioni 40,159,201,400.00 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022, ikiwa Baraza la Madiwani, katika kikao chake kitakachokaa hivi karibuni litapitisha bajeti hii, Halmasahauri ya Wilaya ya Karagwe inatarajiwa kuwa na bajeti yenye ukomo wa kiasi cha bilioni 40,159,201,400.00 ambazo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya na fedha nyingine kutoka serikali kuu na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Aidha ili kuboresha ukusanyaji wa kiasi hicho mapato ya ndani ambapo Halmashauri ya Wilaya inatarajia kukusanya kiasi cha 2, 671,904,000.00 kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ushuru wa kahawa na mazao mengine kama vile maharage, mahindi, ndizi na mazao mengine madogo madogo.
Vyanzo vingine vitahusisha ushuru wa mkaa, mauzo ya mazao ya mkaa, ushuru wa mifugo na vitalu, ushuru wa kuchanja ng’ombe, leseni za vileo, mapato ya Mv. Ruhita, ushuru wa samaki, maombi ya zabuni, usaji wa tax, ushuru wa huduma, ushuru wa uzoaji wa taka ngumu na ushuru wa choo, ushuru wa madini, vibali vya ujenzi, pango la soko, nyumba za Halmashauri ya wilaya, adhabu mbalimbali, ushuru wa malazi, ushuru wa machinjio na ushuru wa asali.
‘’Nimeona mpango wa ujenzi wa Bashungwa Stadium kwa kweli kama mpango huu utafanikiwa Halmashauri ya Wilaya hii itaongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato kutokana na ukweli kwamba wilaya hii ndio inayoongozwa kwa watu kupenda michezo katika mkoa wa Kagera’’, alishauri ndugu Juhudi Felix kwenye kikao hicho.
Ushauri mwingine uliotolewa na wakjumbe wa kikao hicho ilikuwa ni suala la bajeti hii ya Halmashauri ya wilaya kuwa na kifungu cha michezo ili kuchochea shughuli za michezo wilayani hapa.
Ushauri mwingine ilihusu suala la kupeleka miradi kwenye maeneo ambapo wananchi wameonesha nguvu zao pamoja na pendekezo kwa wafanya maamuzi wengine ili mapato yanayotokana na ukusanyaji wa ushuru wa chanjo ya mifugo yaiingizwe kwenye vyanzo lindwa kwani kwa sasa yanapoingizwa kwenye vyanzo visivyolindwa yanaathili suala la bajeti.
Kwa upande wake Wallace Mashanda ambaye ni mjumbe wa kikao hiki kwa wadhifa wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na kukiri uwepo wa upungufu wa magari kama changamoto ya kutokufikia lengo la kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa aliwatoa wasiwasi wajumbe wa kikao hiki kwa kuwaeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na 2021/2022, Halmashauri ya wilaya inatarajia kununua takribani magari matatu ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.