KAMATI YA USHAURI YA WILAYA (DCC) YAPITIA NA KUJADILI RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA 2025/2026
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe; Julius Kalanag Laiser leo tarehe 15.01.2025 ameongoza kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) kupitia na kushauri rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi; Happiness Msanga, Mwenyekiti wa Halmashauri, Viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa Idara, Maofisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Mhe; Laiser ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, akiwakaribisha wajumbe katika kikao hicho maalum cha kujadili bajeti, amewashukuru wajumbe kwa mahudhurio na kuwataka kuwa huru katika kupitia na kujadili mapendekezo ya bajeti na kusisitiza kuwa wazalendo katika kujadili mapendekezo haya ya bajeti kwa ajili ya maslahi mapana ya Halmashauri yetu.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti na mpango wa maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwa mwaka 2025/2026 Ndg; Cyliacus Felician amesema kuwa Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia jumla ya Sh. Bilioni 53.83 kwa mwaka huu wa fedha kwa matumizi mbalimbali ikiwemo ukamilishaji wa zahanati 8 zilizojengwa na wananchi na Uendelezaji wa miradi itakayoiongezea Halmashauri mapato.
Wajumbe walipata nafasi ya kuuliza na kutoa mapendekezo yao kufuatia rasimu ya bajeti iliyowasilishwa ambapo waligusia maswala ya kujenga majengo yanayo kwenda juu (gorofa) kwenye miradi yetu hasa mradi wa ujenzi wa ukumbi wa mikutano ambao umepangwa kutekelezwa katika bajeti hii, ujenzi wa miundo mbinu ya maji Mashuleni na kutenga bajeti kwaajili wa upimaji wa viwanja na kupatiwa hati ili kukomesha migogoro ya aridhi ndani ya jamii.
KARAGWE KAGERA TANZANIA
Anuani ya posta: BOX 20 KARAGWE
Simu: 028-2227148
Simu ya mkononi: 028-2227148
Barua pepe: ded@karagwedc.go.tz ded.karagwedc@kagera.go.tz
Copyright©2017 karagwedc. All rights reserved.